-
UN: Idadi kubwa ya kutisha ya watoto wanaouliwa vitani Sudan
May 07, 2023 03:35Umoja wa Mataifa wiki hii umetahadharisha kuwa idadi kubwa ya watoto wanakufa vitani huko Sudan, na kueleza kuwa ripoti zinaonyesha kuwa watoto saba walikuwa wakiuawa au kujeruhiwa kila saa nchini humo.
-
Mlipuko mkubwa waripotiwa katikati ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum
May 03, 2023 03:37Ripoti zinasema kuwa sauti ya mlipuko mkubwa imesika katikati ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum leo asubuhi.
-
Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kusambaratika hali ya kibinadamu nchini Sudan
May 02, 2023 04:04Martin Griffiths, mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kabla ya kuelekea nchini Sudan kwamba hali ya kibinadamu nchini humo ni mbaya sana kiasi kwamba imefikia kwenye hatua ya kusambaratika kabisa. Amesema, utatuzi wa mgogoro wa Sudan hauwezi kupatikana kutokana na kuendelea vita hivyo.
-
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) waondoa zuio la oparesheni zake huko Sudan
May 01, 2023 22:01Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umetangaza kuwa umeamua kuondoa zuio la oparesheni zake za misaada ya kibinadamu nchini Sudan ambalo liliwekwa kufuatia kifo cha kusikitisha cha mfanyakazi mmoja wa shirika hilo hivi karibuni.
-
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu kuzuka vita vya pande zote nchini Sudan
Apr 29, 2023 22:39Umoja wa Mataifa umeonya juu ya hatari ya kuzuka vita vya upande zote na vya muda mrefu nchini Sudan na athari zake mbaya kwenye mipaka ya nchi hiyo.
-
AU yasisitiza haja ya kumalizwa vita na kuanza mazungumzo nchini Sudan
Apr 28, 2023 22:21Umoja wa Afrika AU umesisitizia haja ya kumalizwa mzozo nchini Sudan na kuanza tena mazungumzo kati ya pande hizo mbili zinazozozana.
-
Mapigano makali yaripotiwa Omdurman, ndege ya abiria ya Uturuki yafyatuliwa risasi
Apr 28, 2023 07:58Mapigano yamezuka tena mepama leo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na milipuko imeendelea kusikika katika baadhi ya maeneo ya mji huo licha ya kuanza kutekelezwa kwa mapatano ya tano ya kusitisha vita tangu mapigano ya ndani yalipoanza kati ya Jeshi la Taifa na Vikosi vya Radiamali ya Haraka (RSF) nchini humo katikati ya mwezi huu.
-
Maelfu ya familia za Wasudani zakimbilia Misri wakihepa mapigano
Apr 28, 2023 03:47Maelfu ya wananchi wa Sudan wamevuka mpaka wa Arqin wa kaskazini mwa nchi hiyo na kuingia Misri wakikimbia mapigano yanayoendelea nchini kwao kati ya Jeshi la Taifa na vikosi vya jeshi la Radiamali ya Haraka (RSF) yaliyoanza katikati ya mwezi huu.
-
Vita Sudan: WHO yasema wagonjwa wengi hawawezi kupata huduma za afya
Apr 27, 2023 07:49Shirika la Afya Duniani WHO linasema mapigano nchini Sudan yamepelekea wagonjwa wengi wenye magonjwa sugu, kama vile ugonjwa wa figo, kisukari na saratani, kutoweza kufikia katika vituo vya afya au dawa wanazohitaji.
-
Upatanishi wa Wazayuni Sudan; kisingizio kingine cha kujipenyeza
Apr 26, 2023 07:28Katika hali ambayo mgogoro wa Sudan pamoja na vita vinaendelea kushuhudiwa, utawala haramu wa Israel umewaalika majerali mahasimu wa Sudan kwenda Tel Aviv kwa ajili ya upatanishi.