-
Iran yakaribisha hatua ya Waarabu ya kuhuisha uhusiano na Syria
Feb 28, 2023 23:10Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepongeza hatua ya nchi za Kiarabu ya kuhuisha na kuimarisha uhusiano na Damascus, akisisitiza kuwa mkondo huo mpya wa kurejea mataifa ya Kiarabu nchini Syria unaonyesha kuporomoka kwa njama za nchi za Magharibi.
-
Rais Bashar al Assad aonana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri mjini Damascus
Feb 27, 2023 22:49Rais Bashar al Assad wa Syria, jana Jumatatu alionana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye ametembelea Damascus kwa ziara ya kikazi, ikiwa ni mkondo mpya wa kurejea nchi za Kiarabu nchini Syria.
-
Spika wa Bunge la Iraq ataka Syria irejeshwe katika nafasi yake katika mataifa ya Kiarabu
Feb 25, 2023 08:17Spika wa Bunge la Iraq ametoa mwito wa nchi ya Syria kurejeshwa katika nafasi iliyokuwa nayo miongoni mwa mataifa ya Kiarabu.
-
Gazeti la Oman: Wakati umewadia wa nchi za Kiarabu kurejea Syria
Feb 21, 2023 07:25Kufuatia safari ya Rais Bashar al Assad wa Syria nchini Oman na mazungumzo aliyofanya mjini Muscat na Sultan Haitham bin Tariq wa nchi hiyo gazeti moja la nchi hiyo limeandika kuwa wakati umewadia kwa nchi za Kiarabu kurudi Syria na kuanzisha tena uhusiano wa kawaida na nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran yalaani hujuma ya kigaidi ya Daesh huko Homs, Syria
Feb 19, 2023 03:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai ya hivi karibuni ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh katika viunga vya mji wa Homs nchini Syria na kusema: "Utawala wa Marekani unafuatilia sera za undumakuwili katika masuala ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi."
-
Raia 53 wauawa katika shambulizi la 'magaidi wa ISIS' Syria
Feb 18, 2023 06:28Kwa akali watu 53 wameuawa katika shambulio linaloaminika kufanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Homs, magharibi mwa Syria.
-
Zaidi ya dazeni mbili za vyama vya Kiarabu vyataka kuondolewa haraka vikwazo dhidi ya Syria
Feb 18, 2023 00:02Zaidi ya dazeni mbili za vyama vya siasa vya Kiarabu vimetaka kuondolewa haraka vikwazo vyote vilivyowekwa na Marekani na washirika wake wa Magharibi dhidi ya Syria, hususan baada ya tetemeko kubwa la ardhi la 7.8 kwa kipimo cha Rishta lililoathiri maeneo ya kaskazini mwa Syria na nchi jirani ya Uturuki.
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran akosoa mienendo ya Wamagharibi kuhusu tetemeko la ardhi nchini Syria
Feb 17, 2023 10:02Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria.
-
Vigingi vya kisiasa vya Magharibi na misaada ya Syria kwa wananchi wa maeneo yanayodhibitiwa na magaidi
Feb 16, 2023 05:29Katika hali ambayo Marekani na nchi za Ulaya zinaingiza masuala ya kisiasa katika masuala ya utumaji misaada ya kibinadamu huko Syria; serikali ya Damascus kwa upande wake inasisitiza kutumiwa misaada wananchi wa Syria katika maeneo yanayoshikiliwa na magaidi.
-
Indhari ya kuenea tishio la Daesh pasi na kutajwa waungaji mkono wake
Feb 13, 2023 22:56Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya katika ripoti yake ya kiduru kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, licha ya hasara na pigo kubwa lililopita kundi la kigaidi la Daesh katika miaka ya hivi karibuni lakini tishio la la kundi hilo la kigaidi lingali linaongezeka kwa ulimwengu.