-
Syria yaitaka Saudi Arabia iache kuunga mkono makundi ya kigaidi
Mar 21, 2018 23:52Katika barua mbili zilizotumwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwenda Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, Damascus imelalamikia mwenendo wa uungaji mkono wa baadhi ya nchi kwa kushirikiana na nchi za Magharibi kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.
-
Umoja wa Mataifa: Hali ya watu wa Afrin, Syria ni mbaya sana
Mar 21, 2018 00:36Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa una wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya raia wa eneo la Afrin huko kaskazini mwa Syria linaloendelea kushambuliwa na jeshi la Uturuki.
-
Ripoti: Kwa akali watoto wa Kiyazidi 120 bado wanashikiliwa na magaidi wa Daesh huko Syria
Mar 20, 2018 01:02Fayhan al-Dakhil, mwakilishi wa kabila la Yazidi katika bunge la Iraq amesema kuwa, kwa akali watoto 120 walio na umri kati ya miaka 10-13, bado wanaendelea kushikiliwa na wanachama wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Syria.
-
Syria yataka askari vamizi wa Uturuki kuondoka mara moja eneo la Afrin
Mar 20, 2018 00:43Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa hivi sasa wa Baraza la Usalama la umoja huo, ikilalamikia uvamizi na jinai za jeshi la Uturuki dhidi ya mji wake wa Afrin na wakazi wake.
-
Wanajeshi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wanashiriki moja kwa moja vitani Syria
Mar 17, 2018 12:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema wanajeshi wa Marekani, Uingereza na Ufaransa wanahusika moja kwa moja katika vita dhidi ya Syria.
-
Rais Assad aahidi kuvunja njama za Wamagharibi dhidi ya Syria
Mar 14, 2018 23:55Rais wa Syria, Bashar al-Assad ameahidi kupambana kikamilifu na njama za Wamagharibi zinazolenga kuvunja umoja wa wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Russia yaionya vikali Marekani kuhusu kushambulia tena Syria, yasema itajibu
Mar 13, 2018 12:22Maafisa wa ngazi za juu wa Russia wameionya vikali Marekani kuwa isithubutu kuishambulia upya Syria kwani matokeo ya chokochoko kama hivyo yatakabiliwa na jibu kali la Russia.
-
Syria: Tishio la US kutuvamia kijeshi linachochea shambulio la silaha za kemikali
Mar 13, 2018 04:09Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amemkosoa vikali mwenzake wa Marekani kwa kutishia kuwa Washington itaishambulia kijeshi nchi hiyo ya Kiarabu kwa tuhuma kuwa serikali ya Damascus imetumia silaha za kemikali, na kusisitiza kuwa kauli za namna hii zinakusudia kuyachochea magenge ya kigaidi yatekeleze hujuma za kemikali dhidi ya raia.
-
Iran: Tutaendelea kuwaunga mkono wananchi walioathiriwa na vita wa Syria na Yemen
Mar 11, 2018 13:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itafanya juhudi zake zote kwa ajili ya kupunguza mateso na masaibu ya wananchi walioathiriwa na vita nchini Syria na Yemen na itaendelea kuwatumia misaada ya kibinadamu.
-
Rais wa Uturuki aiomba NATO ipeleke majeshi yake eneo la Afrin nchini Syria
Mar 11, 2018 03:47Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amelitaka shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO lipeleke majeshi yake katika eneo la Afrin kaskazini mwa Syria.