Iran: Tutaendelea kuwaunga mkono wananchi walioathiriwa na vita wa Syria na Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i41511-iran_tutaendelea_kuwaunga_mkono_wananchi_walioathiriwa_na_vita_wa_syria_na_yemen
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itafanya juhudi zake zote kwa ajili ya kupunguza mateso na masaibu ya wananchi walioathiriwa na vita nchini Syria na Yemen na itaendelea kuwatumia misaada ya kibinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 11, 2018 13:00 UTC
  • Iran: Tutaendelea kuwaunga mkono wananchi walioathiriwa na vita wa Syria na Yemen

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itafanya juhudi zake zote kwa ajili ya kupunguza mateso na masaibu ya wananchi walioathiriwa na vita nchini Syria na Yemen na itaendelea kuwatumia misaada ya kibinadamu.

Mohammad Javad Zarif amesema hayo leo alipoonana na Peter Maurer, mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu hapa Tehran na kujadiliana naye masuala tofauti. 

Mateso ya wananchi wa Yemen

Kwa upande wake, mkuu huyo wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu amesema, shirika hilo lina hamu ya kuendelea kushirikiana na Iran katika masuala muhimu ya kibinadamu na katika jitihada za kuwapunguzia mateso wananchi wenye migogoro ya kibinadamu kama vile wa Syria, Yemen na Iraq.

Pande hizo mbili aidha zimejadiliana njia za kuwasaidia zaidi wananchi wa eneo lenye mapigano la Ghouta Mashariki nchini Syria.

Shirika la Hilal Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran la misaada ya kibinadamu

 

Maudhui nyingine iliyojadiliwa na wawili hao ni kusimamishwa vita haraka nchini Yemen na kutumwa misaada ya madawa na chakula kwa wananchi wa nchi hiyo wanaoishi katika hali mbaya sana.

Pande hizo mbili zimehimiza suala la kuunganishwa juhudi za kimataifa za kuwasaidia binadamu wanaoteseka na vita na kutohusisha misaada hiyo na misimamo ya kisiasa.