Mar 22, 2018 04:22 UTC
  • Syria yaitaka Saudi Arabia iache kuunga mkono makundi ya kigaidi

Katika barua mbili zilizotumwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwenda Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, Damascus imelalamikia mwenendo wa uungaji mkono wa baadhi ya nchi kwa kushirikiana na nchi za Magharibi kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.

Katika radiamali ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria juu ya shambulizi la magaidi hivi karibuni katika viunga vya mji wa Damascus, ambalo lilipelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya raia na hivyo kuamua kutuma barua mbili za malalamiko yake kwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, serikali ya Syria imelaani vikali jinai hizo.

Pande tatu wahusika wa kuzaliwa genge la Daesh na mfano wake

Kadhalika serikali ya Syria imesema kuwa, mashambulizi hayo ni katika mwenendelezo wa jinai za kigaidi za makundi yanayojiita 'Makundi ya Wabeba Silaha ya Misimamo ya Wastani' magenge ambayo yalianzishwa na nchi za kikoloni tangu mwanzoni mwa mgogoro wa Syria hapo mwaka 2011. Itakumbukwa kuwa, katika shambulizi hilo la kigaidi lililolenga soko la mji wa Jaramana, katika viunga vya mji wa Damascus, kwa akali raia 44 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Hujuma za magaidi wa Kiwahabi katika makazi ya raia Syria

Katika barua hizo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria, sambamba na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuheshimu thamani za hati za umoja huo katika fremu ya kuyaepusha mataifa ya ulimwengu na matatizo ya kivita na kufichua malengo halisi ya hujuma hizo kuilenga Syria, imezibebesha pia nchi za kikoloni dhima ya madhara yanayotokana na jinai za makundi ya kigaidi. Kadhalika Syria imeutaka utawala wa Saudi Arabia ukomesha uungaji mkono wake wa kifedha na silaha kwa makundi hayo hatari ya kigaidi nchini humo.

Tags