Maulamaa wa Ahlu Sunna: Muqawama dhidi ya Wazayuni ni wajibu wa kidini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127732-maulamaa_wa_ahlu_sunna_muqawama_dhidi_ya_wazayuni_ni_wajibu_wa_kidini
Zaidi ya wasomi, wanazuoni na wanafikra wa Kisunni wa Iran 1,300 wamesisitiza katika taarifa yao kwa viongozi na vijana wa nchi za Kiislamu kwamba: Kusimama kidete (muqawaama) na kuwapinga makafiri wanaoupiga vita Uislamu na kuunga mkono kambi ya Kiislamu kwa sasa ni wajibu wa kidini na "wajibu wa Kimwenyezi Mungu".
(last modified 2025-06-29T04:31:43+00:00 )
Jun 29, 2025 04:31 UTC
  • Maulamaa wa Ahlu Sunna: Muqawama dhidi ya Wazayuni ni wajibu wa kidini

Zaidi ya wasomi, wanazuoni na wanafikra wa Kisunni wa Iran 1,300 wamesisitiza katika taarifa yao kwa viongozi na vijana wa nchi za Kiislamu kwamba: Kusimama kidete (muqawaama) na kuwapinga makafiri wanaoupiga vita Uislamu na kuunga mkono kambi ya Kiislamu kwa sasa ni wajibu wa kidini na "wajibu wa Kimwenyezi Mungu".

Kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo na ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na vitisho vya moja kwa moja vya utawala wa Kizayuni, wanafikra na wanazuoni zaidi ya 1300 wa Kisuni wa Iran wametoa taarifa na kusisitiza juu ya ulazima wa kuwepo makabiliano ya kila upande na utawala unaoukalia kwa mabavu wa Beitul-Muuqaddas na waungaji mkono wake wa Magharibi.

Imeelezwa katika taarifa hiyo kwamba: "Utawala khabithi wa Kizayuni, ambao mbegu yake ya haramu iliundwa kwa ghasia na kwa kuzingatia sera mbovu za Uingereza na Marekani, ni donda la saratani katika mwili wa nchi za Kiislamu."

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imezitaja jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya wanawake na watoto wa Kipalestina, oparesheni ya tarehe 7 Oktoba  ya Kimbunga cha Al-Aqswa kuwa ni hamasa ya kipekee na kianzio cha kudhoofika utawala wa kijeshi na kiuchumi wa Kizayuni.

Waandishi wa taarifa hiyo wameichukulia hatua ya utawala wa Kizayuni na Marekani katika kuzilenga nchi za Kiislamu na kuwauwa shakhsia kama vile Shahidi Seyed Hassan Nasrullah, Shahidi Seyed Hashim Safiuddin, Shahidi Ismail Haniyeh na Shahidi Yahya Al-Sinwar kuwa ni mfano wa wazi wa uadui dhidi ya kambi ya muqawama.