-
Rais Magufuli Tanzania: Watanzania na Wakenya wasikubali kulaghaiwa kwa maneno ya kuwatenganisha
Jul 05, 2019 11:07Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, amesema kuwa, raia wa Kenya na Tanzania wasikubali kulaghaiwa na kupotoshwa kwa maneno yasiyofaa yanayolenga kuwatenganisha.
-
Hatimaye raia wa Kenya aliyesemekana kutekwa nyara Tanzania, apatikana mjini Mombasa
Jul 02, 2019 09:32Mfanyabiashara wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam Tanzania, amepatikana leo akiwa salama mjini Mombasa nchini Kenya.
-
Zitto Kabwe: Serikali ya Tanzania iliangalie kwa uzito suala la kutekwa raia wa Kenya
Jul 01, 2019 08:13Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya chama cha ACT- Wazalendo nchini Tanzania ameitaka serikali ya nchi hiyo kuliangalia kwa uzito suala la kutekwa nyara raia wa Kenya anayeishi Tanzania, kwa jina la Raphael Ongagi.
-
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Tanzania atembelea eneo walipouliwa Watanzania + Sauti
Jun 30, 2019 12:40Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema imebainika kuwa waliowaua Watanzania 9 kwa kuwapiga risasi na wengine kushambuliwa kwa mapanga ambao ni watu wasiojulikana, walianza chokochoko hizo katika eneo la Kibiti mkoani Pwani baada ya kutimuliwa na na Jeshi la Polisi la Tanzania na wengine wakakimbilia nchi jirani ikiwemo Msumbiji. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu wa Dar es Salaam, Ammar Dachi.
-
Lissu kwenda mahakamani kupinga hatua ya kupokonywa Ubunge
Jun 28, 2019 23:31Baada ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amepoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge, mwanasiasa huyo ambaye anaendelea kuuguza majeraha ya risasi ughaibuni amesema atakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.
-
Zitto Kabwe: Bunge la Tanzania liibane serikali isiendelee kukopa fedha
Jun 27, 2019 03:52Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa kuna umuhimu wa bunge la nchi hiyo kuipangia serikali ya Dar es Salaam kiasi cha fedha inachotakiwa kukikopa ili kupunguza kuongezeka kwa Deni la Taifa sambamba na mikopo hiyo hutumika kikamilifu katika miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
-
SAUTI, Kazi ya ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya Rusumo karibu itakamilika
Jun 24, 2019 13:36Nchi za Rwanda, Tanzania na Burundi zimetangaza kwamba kazi ya kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya mto Rusumo iko mbioni kukamilika.
-
Serikali ya Tanzania: Marufuku watuhumiwa wanawake kukaguliwa na askari wa kiume
Jun 24, 2019 08:47Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola imesema kuwa, mtuhumiwa mwanamke anayefikishwa katika kituo cha polisi hapaswi kukaguliwa na askari wa kiume na badala yake kazi hiyo inatakiwa kufanywa na askari wa kike, mgambo wa kike au mke wa askari aliyepo karibu na eneo la kituo hicho na si vinginevyo.
-
Homa ya Dengue yaua watu wanne nchini Tanzania
Jun 21, 2019 09:55Serikali ya Tanzania leo Ijumaa imetoa kauli Bungeni kuhusu homa ya Dengue na kubainisha kwamba, tangu mwezi Januari hadi Juni mwaka huu 2019, watu wanne wamefariki dunia huku maelfu ya wengine wakiwa wameugua ugonjwa huo.
-
Watanzania: Ongezeko la Shilingi laki moja kwenye pato la mwananchi lipo kwa wabunge
Jun 14, 2019 07:57Raia wa Tanzania wameonyesha kushangazwa na kauli ya serikali ya nchi hiyo kwamba pato la mwananchi wa kawaida liliongezeka kwa Shilingi laki moja zaidi mwaka jana ikilinganishwa na mwaka mmoja kabla, na kusisitiza kwamba pato hilo lipo kwa wabunge pekee.