-
Serikali ya Tanzania: Uchumi wetu ulipanda na kufikia asimia 7.0 mwaka jana
Jun 13, 2019 08:16Serikali ya Tanzania imesema kuwa uchumi wa nchi hiyo ulikuwa na kufikia asilimia 7.0 mwaka jana ukilinganishwa na wa asilimia 6.8 mwaka 2017.
-
Taasisi ya Moyo Muhimbili Tanzania yamshukuru rais wa nchi hiyo + Sauti
Jun 09, 2019 12:21Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya taifa ya muhimbili nchini Tanzania imetoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kwa kuisaidia Taasisi hiyo kupata jengo la Kitengo cha Matibabu ya Moyo kwa Watoto. AMARI DACHI na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Kikao cha Rais Magufuli Tanzania, chaondoka na Waziri wa Viwanda na Kamishna wa TRA
Jun 08, 2019 07:54Kufuatia kikao cha jana cha Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na wafanyabiashara kutoka wilaya zote za nchi hiyo, kiongozi huyo amempiga kalamu nyekundu Joseph Kakunda, Waziri wa Viwanda na Biashara na kumteua mahala pake Innocent Bashungwa kuongoza wizara hiyo.
-
Rais John Magufuli: Natamani kuona mabilionea wengi nchini Tanzania
Jun 07, 2019 08:25Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, amesema kuwa anatamani wakati atakapomaliza muda wake wa uongozi, Tanzania iwe na mabilionea zaidi ya 100.
-
Semina ya kumbukumbu za kufariki dunia Imam Khomeini MA yafanyika Tanzania + Sauti
Jun 02, 2019 23:56Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Bw. Musa Farhang amesema kuwa Imam Khomeini MA alikuwa mfano wa Mwalimu Nyerere katika misimamo yake ya kulitetea taifa la Palestina n.k. Aidha amewahiiza Waislamu kufuata mambo hayo ili waweze kujikwamua kutoka katika ukoloni wa kifikra. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Wananchi wa Tanzania washiriki vikao na maandamano ya Siku ya Quds +SAUTI
May 31, 2019 10:20Mwenyekiti wa Kamati ya Kutetea Haki za Wapalestina nchini Tanzania Abdallah Othman, amemuomba Rais John Pombe Magufuli apaze sauti juu ya suala la kuwaunga mkono Wapelestina, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakidhulumiwa katika ardhi yao.
-
Rais wa Tanzania: Sasa Zimbabwe iondolewe vikwazo kwani uchumi wake umeboreka
May 29, 2019 08:04Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania sambamba na kumpongeza Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, kutokana na hatua madhubuti za kufanya mageuzi ya uchumi katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo.
-
Fatma Karume: Hukumu ya kuzuia wakurugenzi wa serikali kusimamia chaguzi Tanzania, ni kuzuia ushindi wa goli la mkono
May 24, 2019 09:09Fatma Karume, rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amesema kuwa uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuwaengua wakurugenzi wa halmashauri kusimamia chaguzi mbalimbali nchini Tanzania ni sawa na kuzuia ushindi wa goli la mkono katika uchaguzi.
-
Jakaya Kikwete: Licha ya juhudi kubwa za viongozi wa Afrika bado kuna matatizo makubwa ya kiutawala
May 23, 2019 03:52Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa licha ya kuwepo juhudi chanya za viongozi wa Afrika kuonyesha ubunifu wa mipango ya maendeleo, lakini bado kuna tatizo la utawala.
-
Tundu Lissu: Nitarejea Tanzania Septemba 7, sawa na tarehe niliyoshambuliwa
May 22, 2019 10:05Mbunge wa Singida Mashariki wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu amesema kuwa atarejea nyumbani tarehe 7 Septemba mwaka huu kutokea nchini Ubelgiji alikoenda kwa ajili ya kuendelea na matibabu.