Zitto Kabwe: Bunge la Tanzania liibane serikali isiendelee kukopa fedha
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54393-zitto_kabwe_bunge_la_tanzania_liibane_serikali_isiendelee_kukopa_fedha
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa kuna umuhimu wa bunge la nchi hiyo kuipangia serikali ya Dar es Salaam kiasi cha fedha inachotakiwa kukikopa ili kupunguza kuongezeka kwa Deni la Taifa sambamba na mikopo hiyo hutumika kikamilifu katika miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 27, 2019 03:52 UTC
  • Zitto Kabwe: Bunge la Tanzania liibane serikali isiendelee kukopa fedha

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa kuna umuhimu wa bunge la nchi hiyo kuipangia serikali ya Dar es Salaam kiasi cha fedha inachotakiwa kukikopa ili kupunguza kuongezeka kwa Deni la Taifa sambamba na mikopo hiyo hutumika kikamilifu katika miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.

Zitto ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2019 ambao unatazamiwa kupitishwa leo Alhamisi. Kwa mujibu wa Zitto mikopo mingi ambayo inaombwa na serikali, huwa inakwenda kwenye miradi mingine kinyume na malengo ya awali.

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania

“Mwaka huu tunatarajia kukopa Shilingi trilioni 2.3 kama mikopo ya kibiashara lakini sasa hivi serikali inahangaika kutafuta mikopo ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Waziri wa fedha siku za hivi karibuni alikuwa Marekani na timu yake na walikutana na watu wa Benki ya Standard Chartered kuomba mkopo wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) wa Dola bilioni 1.5 kuanzia Morogoro mpaka Dodoma na kwenda mpaka Isaka.” Amesema Zitto. Aidha ameongeza" Juzi nilishangaa, Rais wa Congo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) alikuja nchini na serikali ikampeleka kuangalia SGR na wakazungumzia kuifanya Rwanda kuwa kitovu kwa maana ya reli kwenda huko na Congo kuchukua mizigo Rwanda. Hii maana yake tunaiua Tanzania na Bandari ya Kigoma itakuwa haina maana yoyote.”