-
Zitto Kabwe aufikisha mgogoro wa Spika wa Bunge la Tanzania na CAG katika ngazi ya kimataifa
Jan 10, 2019 12:28Mgogoro ulioibuka kati ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, umezidi kuwa mkubwa baada ya kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Akbar Khan akimtaka kuingilia kat.
-
Mufti wa Tanzania ataka mahujaji wa nchi hiyo watumie Air Tanzania + Sauti
Jan 05, 2019 02:50Viongozi wanaosimamia misafara ya Hija nchini Tanzania wametakiwa kutumia ndege za Shirika la Ndege la Air Tanzania katika msimu wa Hija kama njia ya kuunga mkono jitihada za rais wa nchi hiyo za kuliletea maendeleo Taifa. Ammari Dachi na ripoti kamili kutoka Dar es Salaam.
-
Msumbiji: Raia wa Tanzania na Afrika Kusini ndio wanaoongoza 'al-Shabaab'
Jan 01, 2019 04:46Waendesha Mashitaka nchini Msumbiji wamewataja raia wawili wa Tanzania na mmoja wa Afrika Kusini kuwa miongoni mwa makamanda wa kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo hapo awali lililikuwa linajiita Ahlu Sunna Wal Jamaa, linalofanya hujuma za umwagaji damu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi.
-
Wahajiri 14 wa Ethiopia waaga dunia katika mazingira ya kutatanisha Tanzania
Jan 01, 2019 04:42Polisi ya Tanzania imetangaza habari ya kuaga dunia wahamiaji 14 waliothibitishwa kuwa raia wa Ethiopia mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania.
-
Kamati ya amani Tanzania inayojumuisha Waislamu na Wakristo yaadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS + Sauti
Dec 29, 2018 14:57Kamati ya amani nchini Tanzania ambayo inajumuisha viongozi wa Kiislamu na Kikristo wa madhehebu mbalimbali, imefanya sherehe maalumu za kuadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS na mwaka mpya wa Milaadia. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu Ammar Dachi...
-
Tanzania yawataka wanahabari kutekeleza vyema majukumu yao + Sauti, Video
Dec 24, 2018 03:31Dk Hassan Abbas, msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania amewataka waandishi wa habari nchini humo kutambua haki na kutimiza vyema wajibu wao.
-
Mkutano wa marais wa EAC wafutwa tena
Dec 20, 2018 11:34Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Arusha Tanzania umefutwa kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu.
-
Vyama 6 vya siasa Tanzania vyajadili demokrasia katika mkutano wa Zanzibar+SAUTI
Dec 18, 2018 14:58Viongozi na wanachama waandamizi wa Vyama sita vya siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekutana visiwani Zanzibar hii leo na kujadili juu ya dira ya taifa.
-
Bakwata yaadhimisha miaka 50 ya kuasisiwa kwake+SAUTI
Dec 18, 2018 13:10Huku Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA likitimiza miaka 50 tangu kuasisiwa kwake, MUFTI Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zubeir amewataka waalimu wa elimu ya dini kujifunza elimu zinazoendana na mazingira yao, ikiwemo sayansi na teknolojia.
-
Tanzania na Misri zasaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Stieglers Gorge+SAUTI
Dec 13, 2018 12:31Rais Dkt John Pombe Magufuli wa Tanzania na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, wameshiriki utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme kwenye Mto Rufiji (Stieglers Gorge).