Mkutano wa marais wa EAC wafutwa tena
(last modified Thu, 20 Dec 2018 15:04:24 GMT )
Dec 20, 2018 15:04 UTC
  • Mkutano wa marais wa EAC wafutwa tena

Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Arusha Tanzania umefutwa kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu.

Mkutano huo wa marais wa nchi wanachama wa EAC ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi Sudan Kusini ulitazamiwa kufanyika Disemba 27.

Christophe Bazivamo, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema, "Ni rasmi sasa, mkutano huo hautafanyika Disemba 27 kama ilivyokuwa imepangwa. Tarehe na mahala pa kufanyika mkutano huo wa 20 wa wakuu wa EAC itatangazwa baadaye."

Kikao cha mawaziri wa EAC ambacho hutangulia mkutano wa marais wa jumuiya hiyo ambacho kilitazamiwa kuanza leo Alkhamisi pia kimeakhirishwa.

Bendera za nchi wanachama wa EAC

Duru za habari zimedokeza kuwa, yumkini mkutano huo ukafanyika ima mwezi Februari au Machi mwaka ujao 2019.

Mkutano huu ulitazamiwa kufanyika Novemba 30, lakini ukafutwa baada ya Burundi kusema kuwa haitashiriki.

Wadadisi wa mambo wanasema kuakhirishwa mkutano huu muhimu wa marais wa EAC kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu ni ishara ya kuendelea kuwepo mpasuko mkubwa miongoni mwa nchi wanachama.

 

 

 

Tags