Wizara ya Afya ya Zimbabwe imetangaza kuwa watu wasiopungua 150 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria nchini Zimbabwe katika muda wa miezi miwili iliyopita.
Asilimia 60 ya vifo milioni 5.9 vya watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 5 vilivyotokea mwaka jana katika nchi za Afrika na Asia vilitokana na ugonjwa wa kichomi au nimonia.
Kenya imeteuliwa kuwa makao makuu ya kanda ya Kituo cha Kuratibu Udhibti wa Magonjwa Afrika, CDC-Africa, ili kufuatilia afya ya umma na changamoto katika nchi za Afrika Mashariki.
Wizara ya Afya ya Zanzibar imesema kwa akali watu 45 wamepoteza maisha kutokana na mripuko wa kipindupindu tangu mwezi uliopita wa Machi hadi sasa.
Watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kusambaa ugonjwa wa kipindupindu katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.