Mar 28, 2017 03:54 UTC
  • Makumi ya watu waaga dunia kwa malaria Zimbabwe

Wizara ya Afya ya Zimbabwe imetangaza kuwa watu wasiopungua 150 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa malaria nchini Zimbabwe katika muda wa miezi miwili iliyopita.

Wizara ya Afya ya Zimbabwe ilisisitiza jana Jumatatu kuwa, watu karibu elfu 90 wamegunduliwa kuwa na malaria huko Zimbabwe katika muda wa miezi miwili iliyopita.

Wizara hiyo imeongeza kuwa mvua kubwa zilizonyesha nchini Zimbabwe hivi karibuni ni sababu ya kushuhudiwa ongezeko la ghafla la malaria ambapo idadi kubwa ya watu wameugua ugonjwa huo.

Wizara ya Afya ya Zimbabwe imetaja sababu zilizopelekea kuongezeka wahanga wa maradhi hayo kuwa inatokana na kushindwa kufika wagonjwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu.

Mafuriko yaliyoiathiri Zimbabwe kuanzia Januari mwaka huu 

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na maafisa wa Zimbabwe zinaonyesha kuwa, mvua kubwa zilizonyesha nchini humo zimeuwa watu wasiopungua 46 na kuwafanya wengine 2000 kukosa makazi. Serikali ya Zimbabwe imeomba msaada kwa jamii ya kimataifa ili kukabiliana na mfumuko wa ugonjwa huo. 

Tags