Apr 14, 2016 04:52 UTC
  • Kipindupindu chaua watu kadhaa Zambia

Watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kusambaa ugonjwa wa kipindupindu katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Maafisa wa serikali ya Zambia wamesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu tangu kuanza ugonjwa huo mjini Lusaka mwezi Februari mwaka huu.

Maafisa wa afya wa Zambia wamesema kuwa, maiti za wahanga 11 wa ugonjwa huo zimepatikana majumbani mwao na kwamba wengine watano wamefariki dunia wakiwa katika vuto vya afya. Vilevile kesi 734 za maambuziki ya kipindupindu zimeripotiwa katika mji mkuu wa Zambia.

Wizara ya Afya ya Zambia imeanza kutoa chanzo ya kipindupindu katika baadhi ya maeneo ya jiji la Lusaka.

Wimbi jipya la maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu ambalo lilianzia katika kambi ya wakimbizi wa Kisomali huko mashariki mwa Kenya sasa limeenea zaidi katika nchi kadhaa za Afrika.

Tags