-
Tume ya Uchaguzi: Mshindi wa urais Madagascar ni Andry Rajoelina
Dec 27, 2018 23:51Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Madagascar imetangaza kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Andry Rajoelina ndiye aliyepata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 19, na hivyo ndiye rais wa baadaye wa kisiwa hicho kikubwa zaidi barani Afrika.
-
Nduli wa mauaji ya Waislamu CAR apandishwa kizimbani ICC
Nov 23, 2018 23:16Alfred Yakatom, ambaye wakati fulani alijulikana kwa jina la Rambo kutokana na kufanya mauaji makubwa dhidi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC akikabiliwa na mashtaka 14 ya jinai za kivita na jinai dhidi ya ubinadamu.
-
Israel yakerwa baada ya Madrid kumuenzi mwanaharakati wa Palestina
Sep 30, 2018 23:09Utawala wa Kizayuni wa Israel umeghadhabishwa mno na hatua ya klabu mashuhuri ya soka ya Uhispania ya Real Madrid kumuenzi kwa kumtunuku jezi nambari 9 Ahed Tamimi, binti mwanamapambano wa Kipalestina.
-
Mamia ya wahajiri waokolewa katika maji ya Uhispania
Sep 24, 2018 04:38Jumuiya ya Misaada ya Uokoaji wa Baharini ya Hispania imetangaza kuwa, zaidi ya wahajiri 440 waliokuwa mbioni kuvuka Bahari ya Mediterrania na kuingia barani ulaya wameokolewa majini.
-
Amnesty International yaitaka Uhispania isishirikiane na Saudi Arabia katika jinai zake nchini Yemen
Sep 17, 2018 23:28Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeitaka serikali ya Uhispania iache kuiuzia silaha Saudi Arabia ili isitangazwe kuwa mmoja wa washirika wa utawala wa Aal Saud katika jinai za kivita huko nchini Yemen.
-
Uhispania yawapokea wakimbizi elfu kumi bila ya wazazi wao
Sep 06, 2018 03:23Wizara ya Afya ya Uhispania imetangaza kuwa Madrid inakadiria kuwa wakimbizi 10,000 walio chini ya miaka 18 wapo katika ardhi ya Uhispania peke yao bila ya wazazi wao na imetenga yuro milioni 40 kwa miji ya nchi hiyo inayotaka kuwapokea wakimbizi hao.
-
Dunia yapinga hatua ya Marekani kukata misaada ya shirika la UN linalohudumia wakimbizi wa Palestina
Sep 06, 2018 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania amesema nchi yake inalenga kuongeza maradufu misaada yake kwa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina la Umoja wa Mataifa (UNRWA) baada ya Marekani kukata misaada yake kwa shirika hilo.
-
Uhispania: Marekani haina ustahiki wa kuwa mpatanishi katika kadhia ya Palestina
Sep 05, 2018 03:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania amesema, Marekani imepoteza ustahiki wa kuwa msuluhishi katika suala la Palestina kutokana na kwenda sambamba na misimamo ya Israel.
-
Uhispania kutazama upya mazingira ya kuiuzia silaha Saudi Arabia
Aug 14, 2018 22:02Sambamba na kuendelea uvamizi na hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen ambayo imekuwa ikisababisha mauaji ya kikatili dhidi ya raia na hata watoto wadogo, serikali ya Uhispania imetangaza kuwa, inatazama upya mazingira ya kuiuzia silaha na zana za kijeshi Riyadh pamoja na mataifa mengine yaliyoko katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud.
-
Kutia saini mkataba wa kijeshi na Uhispania; kuendelea siasa za kijeshi za Saudi Arabia
Jul 21, 2018 02:34Saudi Arabia imetiliana saini mkataba mpya wa kijeshi na shirika moja la Uhispani ikiwa ni mwendelezo wa mikataba ya kijeshi ya Riyadh na madola ya Magharibi.