-
Pakistan: Mpango wa Trump kuhusu Ghaza ni tofauti na ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu
Oct 03, 2025 07:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Ishaq Dar amesema mpango wa amani wa vipengele 20 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya Ghaza sio ule ulioidhinishwa na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, ikiwemo Pakistan.
-
Jihadul Islami, Ansarullah zapinga mpango wa Trump-Netanyahu kuhusu Gaza
Oct 01, 2025 07:21Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Jihadul Islami ya Palestina amekosoa vikali mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wenye vipengele 20 wa eti kumaliza vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza, na kuutaja kama "mfumo wa kuendeleza uchokozi na uvamizi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina."
-
Rais wa Colombia: Trump anapasa kufungwa jela kwa jinai za Gaza
Oct 01, 2025 07:19Rais wa Colombia, Gustavo Petro amekosoa vikali sera za mwenzake wa Marekani na kusema kuwa, Donald Trump ni mshiriki wa mauaji ya kimbari huko Gaza na anapaswa kufungwa jela.
-
Russia: Hatutashiriki kwenye mpango wa Trump kuhusu Gaza
Sep 30, 2025 23:03Sambamba na kusisitizia utayarifu wa Russia wa kutatua mgogoro wa Asia Magharibi, Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) amesisitiza kuwa Moscow haitashiriki katika mpango wa Rais wa Marekani juu ya Ukanda wa Gaza.
-
Corbyn: Achilia mbali Ghaza, Tony Blair hafai kuwepo popote katika Mashariki ya Kati
Sep 30, 2025 03:34Kiongozi wa zamani wa Chama cha Leba nchini Uingereza Jeremy Corbyn amesema, waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Tony Blair sio tu hafai kupewa mamlaka ya uliwali wa kuendesha eneo la Ukanda wa Ghaza, lakini hastahili pia kuwepo popote katika Mashariki ya Kati.
-
HAMAS: Tony Blair 'ndugu wa shetani' ni wa kupandishwa kizimbani, si wa kuiongoza Ghaza
Sep 29, 2025 07:16Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani mpango ulioripotiwa kuwa umeandaliwa na Marekani wa kumteua waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair awe liwali wa Ukanda wa Ghaza, na kusisitiza kwamba watu wa Palestina wanao uwezo wa kusimamia mambo yao wenyewe.
-
Ripoti: Tony Blair apendekezwa kuwa Mkuu wa Mamlaka ya Mpito ya uendeshaji wa Ghaza baada ya vita
Sep 26, 2025 22:53Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair yuko kwenye majadiliano ya kuongoza mamlaka ya mpito katika Ukanda wa Ghaza, ikiwa ni sehemu ya mpango unaoungwa mkono na Marekani wa utawala utakaoendesha eneo hilo la ardhi ya Palestina baada ya kuhitimishwa vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa hivi sasa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel.
-
White House: Trump atakutana na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kujadili kadhia ya Ghaza
Sep 23, 2025 03:27Msemaji wa ikulu ya White House Karoline Leavitt ametangaza kuwa rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kufanya mkutano na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kujadili kadhia ya Ghaza.
-
Jihadul-Islami: US na Magharibi hazitaki vita Ghaza vikomeshwe mpaka makundi yote ya Muqawama yaangamizwe
Sep 23, 2025 03:00Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imesema, hakuna mapendekezo mapya ya kusitisha vita Ghaza ambayo yamepokelewa hadi sasa na kuongeza kuwa, Marekani na nchi za Magharibi hazitaki kukomesha vita hivyo hadi pale makundi yote ya Muqawama yanayoupinga utawala wa kizayuni wa Israel, -na si Palestina pekee- bali katika eneo lote, yatakapotokomezwa.
-
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa: Hali ya Ghaza haikubaliki, vita lazima vikome
Sep 23, 2025 03:00Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock ameuambia mkutano wa suluhisho la mataifa mawili uliofanyika makao makuu ya umoja huo jana Jumatatu: "nchi-dola huru ya Palestina lazima ianzishwe".