-
Peskov: Ushindi wa Russia katika operesheni ya kijeshi Ukraine ni suala la kufa na kupona
Apr 14, 2023 03:07Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema, ushindi wa nchi hiyo katika operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine ni suala la kufa na kupona na kwamba kuendelea uingiliaji wa shirika la kijeshi la NATO katika vita vya Ukraine kunarefusha muda wa vita hivyo.
-
Nasser Kanaani: Shughuli za kibiolojia za kijeshi za Marekani huko Ukraine ni kinyume na makubaliano ya kimataifa
Apr 13, 2023 23:02Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa shughuli za kibiolojia za kijeshi zinazotekelezwa na Marekani nchini Ukraine ni kinyume na mapatano ya kimataifa na zinahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kimataifa usioegemea upande wowote.
-
Lavrov: Mazungumzo ya amani kuhusu Ukraine lazima yazingatie 'maslahi na wasiwasi ilionao Russia'
Apr 08, 2023 22:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema mazungumzo yoyote ya amani ya Ukraine lazima yalenge kuanzisha "nidhamu mpya wa dunia" na kuzingatia "maslahi ya Russia na wasiwasi ilionao".
-
Lavrov: Russia na Marekani sasa zimeingia kwenye awamu ya Vita Moto
Apr 06, 2023 03:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amebainisha kuwa, nchi hiyo na Marekani sasa zimeingia katika awamu ya vita moto kutokana na muendelezo wa utumaji silaha kutoka nchi za Magharibi hususan Marekani kuelekea Ukraine kwa kisingizio cha vita katika nchi hiyo.
-
Grossi atahadharisha kuhusu usalama wa kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia
Mar 30, 2023 07:59Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea maafa katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia iwapo kitashambuliwa. Rafael Grossi ametoa indhari hiyo baada ya kukitembelea kituo hicho cha nguvu za nyuklia nchini Ukraine.
-
Amnesty: Vita vya Russia na Ukraine vimeanika undumakuwili uliopo katika haki za binadamu
Mar 28, 2023 06:12Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza katika ripoti yake mpya kuwa kuvamiwa Ukraine na Russia kumeanika undumilakuwili na unafiki uliopo kuhusu haki za binadamu katika uga wa kimataifa, kutokana na jinsi Magharibi ilivyochukua msimamo mkali dhidi ya Russia na kuonyesha "kimya cha uziwi" kwa ukiukaji wa haki za binadamu unaofanyika katika pembe zingine za dunia.
-
Onyo la Russia kuhusu kuzuka vita vya nyuklia kufuatia ongezeko la kutumwa silaha za Magharibi nchini Ukraine
Mar 24, 2023 22:48Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Russia, ameonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia, akisema kuendelea kutumwa silaha nchini Ukraine kunaongeza maradufu uwezekano wa kuibuka hivi karibuni vita vya nyuklia karibu katika eneo.
-
Juhudi za China za kumaliza mgogoro wa Ukraine
Mar 21, 2023 03:22Rais Xi Jinping wa China, amesema kuwa mpango wa nchi yake wa kutatua mzozo wa Ukraine unaakisi maoni ya ulimwengu, na kuwa vipengee 12 vya mpango huo vitaondoa kabisa taathira hasi za mgogoro huo.
-
Undumakuwili wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuhusu jinai za kivita
Mar 19, 2023 04:11Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ambayo inajiona kuwa mahakama ya kwanza ya kudumu ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa mauaji ya halaiki, jinai dhidi ya binadamu, jinai za kivita na uchokozi, Ijumaa iliyopita ilitoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa Rais Vladmir Putin wa Russia.
-
Vassily Nebenzia: Tutafungua mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Ukraine
Mar 18, 2023 10:50Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa ametoa matamshi yake kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Rais na Kamishna wa Haki za Watoto wa Russia akisema Moscow inajiandaa kufungua kesi kuhusiana na Ukraine.