Russia yakaribisha mpango wa China wa amani na Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i96530-russia_yakaribisha_mpango_wa_china_wa_amani_na_ukraine
Russia imeunga mkono mpango wa vipengee 12 uliopendekezwa na China kwa ajili ya kufikia amani kati yake na Ukraine.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 22, 2023 01:40 UTC
  • Russia yakaribisha mpango wa China wa amani na Ukraine

Russia imeunga mkono mpango wa vipengee 12 uliopendekezwa na China kwa ajili ya kufikia amani kati yake na Ukraine.

Mikhail Galuzin Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametangaza kuwa mpango huo wa China wa vipengee 12 uliouwasilisha ili kutatua mgogoro wa Ukraine unaweza kutumiwa kama msingi wa kuanza mazungumzo ya amani kati ya pande mbili. 

Mikhail Galuzin, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia 

Wizara ya Mambo ya Nje ya China hivi karibuni ilizindua mpango wake huo wa vipengee 12 kwa ajili ya kufikia mapatano ya amani ya Ukraine ambao unajumuisha usitishaji vita na kuhitimishwa vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia. 

Katika mpango wake huu, China imesisitiza kuanza kwa mazungumzo ya amani kati ya Moscow na Kiev, kusitisha mapigano, kuhitimishwa vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia, kuchukuliwa hatua za kudhamini usalama wa vituo vya nyuklia,  kuasisi vivuko vya kibinadamu kwa ajili ya  raia, na kuratibiwa hatua mbalimbali za kudhamini usafirishaji wa nafaka nje ya nchi.  

Mpango wa amani wa China pia umesisitiza kuhusu misimamo ya nchi hiyo  ya kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya nchi zote sambamba na kukomeshwa kwa fira za  Vita Baridi". 

China imewasilisha mpango huo wa amani kuhusu Ukraine sambamba na kutimia mwaka mmoja tangu kuanza vita huko Ukraine.