Grossi atahadharisha kuhusu usalama wa kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i95698-grossi_atahadharisha_kuhusu_usalama_wa_kituo_cha_nyuklia_cha_zaporizhzhia
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea maafa katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia iwapo kitashambuliwa. Rafael Grossi ametoa indhari hiyo baada ya kukitembelea kituo hicho cha nguvu za nyuklia nchini Ukraine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 30, 2023 07:59 UTC
  • Grossi atahadharisha kuhusu usalama wa kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea maafa katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia iwapo kitashambuliwa. Rafael Grossi ametoa indhari hiyo baada ya kukitembelea kituo hicho cha nguvu za nyuklia nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Russia walifanikiwa kukiteka kituo cha nguvu za nyuklia cha Zaporizhzhia huko kusini mashariki mwa Ukraine katika miezi ya awali ya vita nchini humo. Hicho ni kituo kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya. 

Pamoja na hayo, kulengwa na mashambulizi maeneo ya kandokando ya kituo hicho na kutuhumiwa pande zote mbili za Russia na Ukraine kuwa zinahusika na mashambulizi hayo kumezidisha wasiwasi kuhusu hatari ya kuvuja mada za radioactive huko mashariki mwa Ukraine. 

Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia 

Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA amesema baada ya kukitembelea kituo cha nyuklia za Zaporizhzhia kwamba ni wazi kuwa hali ya kituo hicho cha nyuklia si tu haijabadilika bali kinyume chake harakati za wanajeshi walioko kandokando ya kituo hicho zimeongezeka. 

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki alitembele kituo hicho cha nyuklia jana Jumatano, hiyo ikiwa ni mara yake ya pili tangu kuanza vita huko Ukraine.  

mwezi Septemba mwaka jana Grossi alikitembelea kwa mara ya kwanza kituo cha nyuklia huko kusini mashariki mwa Ukraine.  Kituo hicho ni cha zama za Umoja wa Kisovieti;  na Ukraine inahitaji kituo hicho kifanye kazi ili kudhamini mahitaji ya umeme ya nchi hiyo. 

Eneo la Zaporizhzhia ni kati ya maeneo ambayo mwezi septemba mwaka jana Russia iliitisha kura ya maoni na kuyaunganisha na ardhi yake na inaonekana kuwa Moscow haina nia ya kufikia maelewano na upande wa Ukraine katika suala hili.