-
Indhari ya Russia kuhusu kufutwa makubaliano ya JCPOA na taathira zake mbaya
May 05, 2018 07:39Serikali ya Russia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni utaratibu ulio na mlingano weenye manufaa ya pande zote na kutahadharisha kuwa kuvunjwa makubaliano hayo kutakuwa kwa madhara. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Russia, kuvurugwa mlingano unaolegalega wa kimaslahi ndani ya makubaliano ya JCPOA kutakuwa na taathira kuu kwa usalama wa kimataifa na muundo unaopiga marufuku uenezaji wa silaha za nyuklia.
-
Indhari ya Amnesty International kwa EU juu ya ushiriki wake katika mashambulizi ya anga ya Marekani
Apr 29, 2018 08:45Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limezionya nchi za Ulaya ambazo zina mpango wa kushiriki katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ya Marekani, kutokana na kutekelezwa mauaji ya raia katika hujuma hizo.
-
Iran: Tutasimama kidete kukabiliana na vikwazo vyovyote vile
Apr 28, 2018 23:07Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna kikwazo chochote kitakacholenga manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu kitakachoachwa vivi hivi hivi bila ya kutumia uwezo wetu wote kupambana nacho.
-
Wahajiri 11 wa Kiafrika wamekufa maji katika pwani ya Libya
Apr 23, 2018 03:15Kwa akali wahajiri 11 wa Kiafrika wameripotiwa kufariki dunia baada ya boti yao kuzama katika maji ya pwani ya magharibi mwa Libya, wakati wakiwa safarini kuelekea Ulaya.
-
Jibu madhubuti la Russia kwa hatua ya nchi za Umoja wa Ulaya
Mar 31, 2018 10:14Serikali ya Russia ilitangaza jana Ijumaa kuwa itawafukuza wanadiplomasia 59 wa nchi 23 tofauti walioko nchini humo. Uamuzi huo wa Moscow umechukuliwa kujibu hatua ya nchi hizo ya kuwafukuza kwa mpigo wanadiplomasia wa Russia. Katika jibu na radiamali yake kwa hatua ya kufukuzwa wanadiplomasia wake, serikali ya Moscow imechukua uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomasia 41 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
-
Utafiti: Mamilioni kuhama Afrika na kuelekea Marekani na Ulaya
Mar 23, 2018 09:37Watafiti wanasema kuwa karibu watu milioni 1.5 wameondoka katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika na kuelekea Ulaya na Marekani tangu mwaka 2010, huku mamilioni ya wengine wakifanya mipango ya kufuata nyao za wenzao.
-
Ujerumani yamkosoa Trump juu ya hatari ya vita vya kibiashara na EU
Mar 06, 2018 23:42Msemaji wa Serikali ya Ujerumani ameikosoa Marekani juu ya uwezekano wa kutokea vita vya kibiashara kufuatia hatua ya Washington kuongeza kiwango cha ushuru wa forodha kwa bidhaa za Ulaya.
-
Rouhani: Pande zote zitajuta iwapo makubaliano ya nyuklia ya Iran yatavunjika
Mar 05, 2018 23:26Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pande zote husika zitajuta iwapo makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yatasambaratika, katika hali ambayo Marekani inafanya jitihada za kuyafelisha mapatano hayo na kutoa vitisho vya kujiondoa kwenye makubaliano hayo kila mara.
-
Waislamu wapinga azma ya Iceland ya kupiga marufuku kutahiriwa vijana wa kiume
Feb 25, 2018 12:15Viongozi wa Kiislamu nchini Iceland wamepinga vikali muswada wa sheria inayotaka kupiga marufuku vijana wa kiume kutahiriwa katika nchi hiyo ndogo ya bara Ulaya.
-
China yauonya Umoja wa Ulaya kwa hatua yake mbaya dhidi ya biashara zake
Feb 11, 2018 03:57Serikali ya China imeuonya Umoja wa Ulaya kutokana na siasa mbaya za umoja huo dhidi ya Beijing na kusisitiza kwamba mienendo hiyo inaweza kuvuruga mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi hiyo na umoja huo.