-
UNICEF: Watoto wameathiriwa zaidi na vita katika Ukanda wa Gaza
Jan 29, 2025 22:27Mfumo wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto ndio walioteseka na kuathirika zaidi na vita vya Gaza kkuliiko matabaka mengine katika Ukkanda huo.
-
Uungaji mkono wa Marekani kwa hatua ya utawala wa Kizayuni dhidi ya UNRWA
Jan 29, 2025 08:47Rais Donald Trump wa Marekani ameendeleza uungaji mkono wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kufuta idhini ya serikali ya Biden kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), na kutangaza kuwa anaunga mkono uamuzi wa utawala huo wa kufunga ofisi ya UNRWA huko Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu.
-
Huduma mpya za Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Jan 28, 2025 23:05Katika siku za mwanzo za muhula wake wa pili wa uongozi, Donald Trump, rais mpya wa Marekani, kwa mara nyingine tena amefuata njia ile ile aliyopitia katika muhula wa kwanza wa uongozi wake. Katika muhula wa kwanza, Trump alitoa uungaji mkono mkubwa na ambao haujashuhudiwa kwa utawala wa Kizayuni na kuchukua hatua mpya sambamba na kuiunga mkono Israel na kuwapinga Wapalestina. Vitendo na misimamo hii imekutana na majibu chanya kutoka Tel Aviv.
-
Mashirika ya haki za binadamu ya Poland: Mkamateni waziri mhalifu wa Israel
Jan 28, 2025 04:29Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Poland yametoa wito wa kukamatwa Waziri wa Elimu wa Israel ambaye yuko safarini nchini humo.
-
Hamas: Wananchi wa Palestina watabaki katika ardhi yao
Jan 27, 2025 03:51Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa wananchi wa Palestina wako imara katika ardhi yao na mpango wowote wa kuwahamisha utafeli. Amesisitiza kuwa: Wapalestina watabaki katika ardhi yao.
-
UNRWA yajibu vitisho vya Israel vya kusimamisha shughuli za shirika hilo la kimataifa
Jan 27, 2025 03:48Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa radiamali yake kwa vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kusitishwa shughuli za shirika hilo la Umoja wa Mataifa huko Baitul Muqaddas Mashariki.
-
UNIFIL yasisitiza kuondoka Lebanon wanajeshi wa Israel
Jan 27, 2025 03:38Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon (UNIFIL) kimetaka kuondoka kikamilifu wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko kusini mwa Lebanon.
-
Makumi wauawa na kujeruhiwa baada ya askari wa Israel kuwafyatulia risasi raia kusini mwa Lebanon
Jan 26, 2025 08:07Vikosi vya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel vimewafyatulia risasi raia wa Lebanon wanaorejea makwao katika miji ya kusini mwa nchi hiyo, na kuua watu wasiopungua 11 na kuwajeruhi wengine 83.
-
HAMAS kuwaachia askari 4 wanawake wa Israel kwa Wapalestina 200 akiwemo kamanda wa Muqawama
Jan 25, 2025 03:09Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kamanda maarufu wa Palestina ataachiliwa leo ikiwa ni sehemu ya mabadilishano ya pili ya wafungwa na utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza kuanza kutekelezwa wiki iliyopita.
-
Israel haitaondoa askari wake kusini mwa Lebanon kama ilivyoafikiwa, Marekani yaiunga mkono
Jan 25, 2025 02:44Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halitaondoka kusini mwa Lebanon utakapomalizika muhula uliowekwa wa siku 60 kesho Jumapili kulingana na makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa kati ya Israel na harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah.