UNICEF: Watoto wameathiriwa zaidi na vita katika Ukanda wa Gaza
Mfumo wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto ndio walioteseka na kuathirika zaidi na vita vya Gaza kkuliiko matabaka mengine katika Ukkanda huo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limebainisha katika taarifa yake kuwa watoto wameteseka zaidi katika vita huko Gaza na wanahitaji uangalizi wa haraka ili kukabiliana na mahitaji yao ya haraka, kuhakikisha afya zao, elimu na ustawi wao.
Taarifa ya UNICEF imeeleza kuwa, zaidi ya malori 350 yaliyobeba misaada ya kibinadamu ya shirika hili yameingia Gaza ikiwa ni katika juhudi za kukidhi mahitaji ya wakazi wa Gaza hususan watoto.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limetangaza katika taarifa hiyo kwamba malori ya kubeba maji, vifaa vya afya, matibabu ya utapiamlo, nguo na misaada mingine muhimu ya kibinadamu yamefika kupitia vivuko kaskazini na kusini mwa Ukanda wa Gaza na kusambazwa kwa familia zinazohitaji.
Mfuko wa Kudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) hivi karibuni ulitangaza kuwa, watoto wasiopungua 15,000 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu utawala wa Kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vyake dhidi ya ukanda huo Oktoba 7 mwaka 2023.
Katika upande mwingine, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umeonya kuwa karibu watoto wote milioni 1.1 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili na wanahitaji msaada wa kisaikolojia.