-
Hamas: Tumejenga upya uwezo wetu kwa vita vyovyote vya siku zijazo
Mar 05, 2025 04:13Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS amesema kuwa, ingawa uamuzi wa kuanzisha tena vita kwa sasa unaonekana uko mbali, lakini harakati hiyo tayari imejenga upya uwezo wake wa kijeshi ili kukabiliana na vita vyovyote vile vya siku za usoni.
-
Filamu kuhusu Israel inavyowatimua Wapalestina katika ardhi yao yashinda tuzo ya Oscar
Mar 04, 2025 03:00Filamu kuhusu utawala haramu wa Israel unavyowatimua Wapalestina katika ardhi yao, imeshinda tuzo ya Oscar na wakurugenzi wake wametoa wito kwa ulimwengu kusaidia kumaliza mgogoro huo na kuishutumu Marekani kwa kuzuia kufikiwa utatuzi.
-
Misaada ya kijeshi na silaha ambayo haijawahi kutolewa mfano wake ya serikali ya Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Mar 04, 2025 02:58Sambamba na Marekani kukata misaada yake kwa Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, siku ya Jumapili alitumia mamlaka ya dharura aliyonayo kisheria kupitisha mpango wa utoaji msaada wa shehena ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 4 kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mamlaka ya Ndani ya Palestina yataka walimwengu waishinikize Israel
Mar 03, 2025 02:23Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeonya juu ya matokeo mabaya ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuitaka jamii ya kimataifa kuulazimisha utawala wa Kizayuni utekeleze majukumu yake ya kibinadamu.
-
Israel yakiri rasmi kushindwa katika oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa
Feb 28, 2025 07:31Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa, katika mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka 2023 lilishindwa kuwahami walowezi wa utawala huo wanaoishi katika maeneo jirani na Gaza; na kwamba lilifeli katika masaa ya awali mkabala wa mashambulizi ya Hamas.
-
Baqaei: Kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa Israel nchini Syria
Feb 27, 2025 11:47Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa utawala haramu wa Israel nchini Syria
-
Israel inakusudia nini kwa mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya Syria?
Feb 27, 2025 09:58Utawala wa Kizayuni wa Israel Jumatano Februari 26 ulishambulia mara kadhaa maeneo mbalimbali ya Syria na kuua na kujeruhi watu kadhaa.
-
Mashtaka dhidi ya utawala wa Biden katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
Feb 27, 2025 02:36Taasisi ya "Demokrasia kwa ajili ya Ulimwengu wa Kiarabu Sasa" (DAWN), imefungua mashtaka dhidi ya Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden na mawaziri wake wawili yaani waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Anthony Blinken na waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo Lloyd Austin katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ikiitaka ianzishe uchunguzi dhidi ya viongozi hao kutokana na kusaidia uhalifu wa kivita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
HAMAS: Mwafaka umefikiwa kuhusu Wapalestina 620 ambao Israel ilichelewesha kuwaachia huru
Feb 26, 2025 12:58Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, ujumbe wake umehitimisha ziara yake katika mji mkuu wa Misri Cairo na umefikia makubaliano na wapatanishi ya kutatuliwa ucheleweshaji uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuwaachilia huru wafungwa Wapalestina ambao ilipasa waachiliwe siku ya Jumamosi iliyopita kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili.
-
Misri yakataa pendekezo la Wazayuni la kuitawala Gaza kwa miaka 8
Feb 26, 2025 06:40Cairo imekataa pendekezo la maafisa wa utawala za Kizayuni wa Isarel wanaotaka serikali ya Misri isimamia mamlaka ya Ukanda wa Gaza kwa miaka 8 hadi 15.