-
Uturuki: Uamuzi wa Marekani unakinzana na moyo wa umoja na ushirikiano
Jul 18, 2019 08:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ametoa radiamali kuhusiana na uamuzi wa Marekani wa kuiondoa serikali ya Ankara kwenye mpango wa kununua ndege za kivita za F 35 na kusema kuwa, uamuzi huo wa Washington unakinzana na moyo wa umoja na ushirikiano baina yao.
-
Kauli hasi ya Trump kwa sababu ya kupatiwa Uturuki vifaa vya mfumo wa makombora wa S-400 wa Russia
Jul 17, 2019 21:50Uamuzi wa Uturuki wa kununua mfumo wa kisasa wa makombora ya ulinzi wa anga wa S-400 kutoka Russia umezusha mikwaruzano mikubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa katika uhusiano wa Uturuki na Marekani.
-
Maelfu waandamana Uturuki kuilaani Marekani, Israel
Jul 16, 2019 22:50Maelfu wa wananchi wa mji wa Adana wa kusini mwa Uturuki wamefanya maandamano ya kuilaani Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Uturuki kuendelea na mpango wa kuchimba mafuta na gesi Bahari ya Mediterania licha ya upinzani wa EU
Jul 16, 2019 22:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesisitiza kuwa, nchi hiyo itaendelea na mpango wake wa kutafuta mafuta na gesi mashariki ya bahari ya Mediterania licha ya agizo la Umoja wa Ulaya kuitaka isimamishe mpango huo.
-
Uturuki: Mfumo wa makombora wa S-400 si chaguo, ni hitajio la lazima kwa usalama wetu
Jul 14, 2019 08:52Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar ameiambia Marekani kuwa uamuzi wa nchi yake wa kununua mfumo wa ulinzi wa makombora wa S-400 kutoka Russia hautokani na chaguo la ufadhilishaji, bali ni hitajio la lazima kwa usalama wa nchi hiyo kwa sababu inakabiliwa na tishio kubwa.
-
Mwanasiasa nchini Misri: Nchi za Kiarabu zifanye mazungumzo na Iran na Uturuki
Jul 13, 2019 02:43Mwanadiplomasia na mgombea wa zamani wa uchaguzi wa rais nchini Misri, Abdullah al-Ashaal amezitaka nchi za Kiarabu zifanye mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki.
-
Uturuki yaanza kupokea mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Russia
Jul 12, 2019 20:38Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Russia licha ya makelele na vitisho vya Marekani.
-
Duru mpya ya mazungumzo ya Astana kuhusu Syria kuanza tena
Jul 11, 2019 21:55Duru mpya ya mazungumzo ya Astana kuhusu mgogoro wa Syria inatazamiwa kuanza mapema mwezi ujao wa Agosti huko Nur-Sultan mji mkuu wa Kazakhstan.
-
Mbunge wa Uturuki aionya Marekani juu ya kuishambulia kijeshi Iran
Jun 28, 2019 23:36Öztürk Yılmaz, mbunge wa Uturuki, ameionya Marekani juu ya kuchukua hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inayoweza kuibua mapigano katika eneo.
-
Erdogan asisitiza tena juu ya ulazima wa kuanzishwa eneo salama huko Syria
Jun 26, 2019 21:51Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki kwa mara nyingine tena amesisitiza juu ya udharura wa kuanzishwa eneo salama kaskazini mashariki mwa Syria na karibu na mpaka wa Uturuki kwa lengo la kuwarejesha nchini kwao wakimbizi wa Syria.