-
Kanisa la Methodist Afrika lajiunga na harakati ya kuuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni
Oct 12, 2019 08:45Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa Palestina ametangaza kuwa Kanisa la Methodist la Kusini mwa Afrika (MCSA) limejiunga na Harakati ya Kimataifa ya Kususia na Kuiwekea Vikwazo Israel- Boycott, Divestment and Sanctions- (BDS), kutokana na jinai za utawala huo wa Kizayuni dhidi ya taifa la Palestina.
-
Vikwazo vya Marekani; uchokozi wa wazi dhidi ya nchi nyingine
Oct 06, 2019 07:42Mashinikizo ya Marekani dhidi ya Cuba na Venezuela yanazidi kushtadi, huku nchi hizo zikiwa zinaendelea kushikamana na malengo yao na kusisitizia juu ya kuimarishwa ushikamano wao.
-
Trump na ahadi zake bandia za kuiondolea Iran vikwazo baada ya kufanyika mazungumzo
Sep 30, 2019 08:36Baada ya kuiondoa nchi yake kwenye mapatano ya nyuklia mwezi Mei mwaka jana na kisha kuiwekea vikwazo vikali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika miezi ya hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha hamu kubwa ya kutaka kufanya mazungumzo na Iran ambapo baada ya kufanya mazungumzo na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kulienea fununu za uwezekano wa kukutana marais wa Iran na Marekani kando ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
-
Sheikh Nabil Qaouk: Vikwazo vya Marekani havijawa na taathira yoyote kwa Hizbullah
Sep 28, 2019 22:59Mjumbe wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya harakati hiyo havijawa na taathira na kwamba, vikwazo hivyo ni matokeo ya kukata tamaa Washington.
-
Duru mpya ya hujuma za vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi zingine
Sep 28, 2019 04:29Marekani ina rekodi kubwa zaidi ya kutumia aina mbali mbali za vikwazo dhidi ya nchi zingine kwa ajili ya kufikia malengo ya siasa zake za nje. Ushadidishaji vikwazo unaofanywa na Washington katika kipindi cha urais wa Donald Trump umekuwa ukipingwa na kulaaniwa kimataifa. Pamoja na hayo kinachoendelea kushuhudiwa kila uchao ni kutangazwa vikwazo vingine vipya vya Marekani dhidi ya nchi zingine duniani.
-
Rouhani: Vikwazo vya kikatili vya Marekani vimeongeza mshikamano nchini Iran
Sep 26, 2019 09:02Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya kikatili vya Marekani dhidi ya Tehran vimeshindwa kufikia malengo yake, na badala yake vimeongeza mshikamano miongoni mwa wananchi wa Iran.
-
China yalaani vikwazo vya Marekani dhidi yake kwa kununua mafuta ya Iran
Sep 26, 2019 08:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China amekosoa vikali hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo vipya nchi hiyo ya Asia kwa kuendelea kununua mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kukiri Marekani kwamba vikwazo vyake dhidi ya Iran vimefika kileleni na vimefeli
Sep 23, 2019 23:18Baada ya kujitoa bila sababu katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia maarufu kwa jina la JCPOA na kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyokuwa vimeondolewa baada ya mapatano hayo, bali kuongeza vikwazo vikubwa zaidi ambavyo havijawahi kutokea mfano wake, leo hii serikali ya Donald Trump ya Marekani imelazimika kukiri kuwa vikwazo vyake hivyo vimeshindwa kuzaa matunda yaliyotarajiwa.
-
Dakta Zarif: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vinafunga milango yote ya mazungumzo
Sep 22, 2019 09:25Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye ameelekea New York Marekani kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua mpya ya Marekani dhidi ya Iran.
-
Zarif: Vikwazo vya Marekani vinawalenga wananchi wa kawaida wa Iran
Sep 19, 2019 09:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani ya kutangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, kushadidishwa ugaidi huo wa kiuchumi kwa mara nyingine kumeonesha namna Washington inavyowalenga Wairani wa kawaida.