Mayahudi wa Afrika Kusini waususia kitaaluma utawala wa Kizayuni
Karibu wasomi 70 wa Kiyahudi wa nchini Afrika Kusini wameususia kitaaluma utawala ghasibu wa Kizayuni.
Wasomi hao 69 Wayahudi wa Afrika Kusini wamevisusia Vyuo Vikuu vya utawala wa Kizayuni kutokana na jinai zinazofanywa na utawala huo wa kibaguzi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Wsomi tajwa huku wakiwa pamoja na shaksia wengine Wayahudi wa Afrika Kusini watajika kiutamaduni na kielimu wameandika barua na kuunga mkono uamuzi uliochukuliwa Jumapili tarehe 15 mwezi huu na timu ya uongozi ya Chuo Kikuu cha mjini Cape Town ambacho kinafahamika kama Chuo Kikuu cha ngazi ya juu zaidi barani Afrika wa kuvisusia kimasomo na kitaalumu vituo vya elimu na utafiti vyenye mfungamano na utawala wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Wasomi hayo Wayahudi wa Afrika kusini wamewataka viongozi wa Chuo Kiku cha Cape Town kujiepusha kuanzisha uhusiano wa kielimu, kiutafiti na kifedha na taasisi za kitaaluma huko Israel na nyinginezo ambazo zinakiuka haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. Kundi hilo la shakhsia watajika wa Afrika Kusini tayari limejiunga na harakati kubwa zaidi ya kimataifa ya kuususia utawala wa Kizayuni kote duniani katika nchi za Uingereza, Canada, Ulaya, Australia, Brazil na Argentina.