-
Araqchi: Vikwazo vipya vya US vinalenga kuisambaratisha JCPOA
Aug 03, 2017 02:55Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kusaini sheria ya vikwazo vipya dhidi ya Tehran ni njama ya Washington ya kutaka kusambaratisha makubaliano ya nyuklia ya Vienna yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA.
-
Trump asaini mswada wa vikwazo dhidi ya Iran, Russia na Korea Kaskazini
Aug 02, 2017 22:04Rais Donald Trump wa Marekani amesaini kuwa sheria mpango wa vikwazo uliopitishwa na Bunge la Wawakilishi na Seneti ya nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na Korea Kaskazini.
-
Nchi nne za Kiarabu zang'ang'ania msimamo wao wa kuendeleza vikwazo dhidi ya Qatar
Jul 30, 2017 23:57Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi nne za Kiarabu zilizovunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na kuiwekea vikwazo nchi hiyo wametoa taarifa wakitilia mkazo misimamo ya hapo kabla ya nchi hizo na kuendelezwa vikwazo dhidi ya Doha.
-
Russia yajibu Marekani, yapunguza idadi ya wanadiplomasia wa Marekani na kuzuia mali zao
Jul 28, 2017 21:51Katika kujibu hatua ya vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia, serikali ya Moscow imetoa amri ya kupunguzwa idadi ya wanadiplomasia wa nchi hiyo nchini humo sambamba na kuzuia baadhi ya mali za kidiplomasia za maafisa hao.
-
Syria yakosoa kuendelezwa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi yake
Jul 28, 2017 21:51Bashar Jaafari, Mwakilishi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amelaani mwendelezo wa vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi yake na kusema kwamba vikwazo hivyo vimelemaza kabisa shughuli za mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini humo.
-
Kamal Kharrazi: Hatua za kihasama za Marekani dhidi ya Iran si jambo jipya
Jul 28, 2017 02:59Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Iran amesema: Hatua za kihasama za Rais wa Marekani dhidi ya Iran ni siasa zilizoanza tangu mwaka 1979 wakati wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na zinaendelea hadi sasa.
-
Dakta Larijani: Iran imejiandaa kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani
Jul 27, 2017 23:03Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Iran imejiandaa kikamilifu kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Rais Hassan Rouhani: Iran itatoa jibu kali kwa Marekani
Jul 26, 2017 09:23Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran itatoa jibu kali kwa hatua ya Marekani ya kupasishwa vikwazo vipya dhidi ya taifa hili.
-
Nchi nne za Kiarabu zashadidisha vikwazo vyao dhidi ya Qatar
Jul 25, 2017 09:46Nchi nne za Kiarabu zilizovunja uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar na kuiwekea vikwazo nchi hiyo ya Kiarabu leo zimetoa orodha mpya ya majina ya taasisi na shakhsia zinaodai kuwa wana mfungamano na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Qatar.
-
Russia yalaani hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo vipya Iran
Jul 21, 2017 03:14Mkuu wa Idara ya Kuzuia na Kudhibiti Silaha iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Mikhail Ulyanov amelaani hatua ya kiuhasama ya Marekani katika kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vipya na kusema kuwa, vikwazo hivyo havijazingatia sheria zozote zile.