Kutekelezwa vikwazo mpya vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32800-kutekelezwa_vikwazo_mpya_vya_umoja_wa_ulaya_dhidi_ya_russia
Umoja wa Ulaya umeanza kutekeleza vikwazo vipya dhidi ya Russia kuhusiana na mzozo wa peninsula ya Crimea.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 06, 2017 23:14 UTC

Umoja wa Ulaya umeanza kutekeleza vikwazo vipya dhidi ya Russia kuhusiana na mzozo wa peninsula ya Crimea.

Katika fremu hiyo Kamisheni ya Ulaya na kwa kuzingatia hatua iliyozusha mjadala mkubwa ya kuhamisha mitambo ya gesi iliyotengenezwa na shirika la Ujerumani la 'Siemens' na kuipeleka katika eneo la Crimea, Ijumaa iliyopita iliwawekea vikwazo shakhsia watatu na mashirika mengine matatu ya Russia.

Itakumbukwa kuwa baada ya kufanyika kwa kura ya maoni eneo la Crimea na hatimaye kuliunganisha eneo hilo na Russia hapo mwaka 2014, Umoja wa Ulaya uliiwekea vikwazo serikali ya Moscow na hadi sasa bado vikwazo hivyo vingali vinaendelea kutekelezwa. Miongoni mwa watu ambao walijumuishwa katika orodha nyeusi ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya ni Andrei Cherezov, Naibu Waziri wa Nishati wa Russia.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa ikisisitiza hamu ya nchi hiyo ya kudumishwa ushirikiano wa kiuchumi na Umoja wa Ulaya na kusema kuwa Moscow nayo inalinda haki yake ya kulipiza kisasi kuhusiana na vikwazo  hivyo mpya vya EU. Kwa mtazamo wa Moscow, vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia ni vya kiuhasama na visivyo na msingi wowote.

Inaonekana kuwa, hivi sasa suala la kuiwekea vikwazo Russia limekuwa chanzo cha kuchafuliwa zaidi mahusiano kati ya Moscow na Umoja wa Ulaya. Hii ni katika hali ambayo katikati ya mwezi Juni mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulijadidisha vikwazo vya huko nyuma dhidi ya Russia viliyowekwa mwaka 2014 baada ya hatua ya Moscow ya kuliunganisha eneo la Cremia na ardhi ya nchi hiyo. EU imepigilia msumari wa vikwazo hivyo kwa kuongeza vikwazo vingine juu yake, hatua ambayo kwa mtazamo wa Russia ni harakati ya kiuadui..

Utunishianaji misuli kati ya Marekani na Russia

Kwa upande mwingine ni kwamba pamoja na kuwa Umoja wa Ulaya unataka kuendelezwa mashinikizo zaidi dhidi ya Moscow, lakini umepinga vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Russia. Hususan kwa kuzingatia kwamba vikwazo hivyo vinaweza kuwa na taathira hasi kwa miradi ya mafuta na gesi na mashirika mbalimbali ya Ulaya.

Kuhusiana na suala hilo, Jean-Claude Juncker, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya sambamba na kubainisha kwamba umoja huo unaviona vikwazo vipya vya Washington dhidi ya Russia kuwa ni sehemu ya siasa za viwanda za Marekani, amesema kuwa EU itatetea maslahi yake ya kiuchumi dhidi ya Marekani. Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia vimeijumuisha pia sekta ya usafirishaji wa gesi kwenda barani Ulaya.

Ukweli ni kwamba, Umoja wa Ulaya sambamba na kuendeleza siasa za vikwazo dhidi ya Russia, lakini wakati huo huo unataka kuchungwa mistari myekundu katika uwanja huo, katika hali ambayo Washington umeiwekea vikwazo Moscow kwa kufuata maamuzi yake binafsi na bila kuzingatia maslahi ya Ulaya.

Jean-Claude Juncker Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya EU

Den Lazar mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema: "Vita vipya vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Russia vinatishia uhusiano wa nchi hiyo nana Ujerumani. Ii kulinda maslahi na hali bora y watu wao, viongozi wa nchi za Ulaya wanalazimika kuchukua maamuuzi ya ama kukabiliana na hatua za Marekani au kushirikiana na Washington katika kuiwekea vikwazo Russia."