-
Mnangagwa aapishwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe, aahidi kulijenga upya taifa
Nov 24, 2017 12:28Emmerson Mnangagwa, Makamu wa Rais wa Zimbabwe aliyefutwa kazi na Robert Mugabe wiki chache zilizopita ameapishwa hii leo kuwa rais mpya wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, huku akiahidi kulijenga upya taifa hilo linalokabiliwa na mtikisiko mkubwa wa kiuchumi.
-
Rais mtarajiwa wa Zimbabwe kuapishwa leo
Nov 24, 2017 04:27Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kutawazwa leo Ijumaa, ikiwa ni siku tatu tu baada ya mtangulizi wake Robert Mugabe kuachia ngazi kwa mashinikizo ya jeshi na chama chake cha Zanu-PF.
-
Hatimaye Rais Mugabe wa Zimbabwe asalimu amri, akubali kujiuzulu
Nov 21, 2017 10:14Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe hatimaye amesalimu amri na kukubali kujiuzulu. kufutia mashinikizo ya kila upande ya kumtaka aachie madaraka.
-
Mugabe apewa kinga ya kutoshtakiwa, adhaminiwa usalama wake ndani ya Zimbabwe
Nov 23, 2017 10:57Aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepewa kinga ya kutoshtakiwa sambamba na kudhaminiwa usalama wake ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Kujiuzulu Mugabe na mustakabali wa kisiasa wa Zimbabwe
Nov 22, 2017 23:57Hatimaye baada ya takribani wiki moja ya changamoto, mivutano na uingiliaji wa jeshi hatimaye Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ameng'atuka madarakani. Mugabe amechukua hatua hiyo baada ya Bunge kuanzisha mchakato wa kumsaili kwa lengo la kumuuzulu.
-
Mnangagwa arejea Zimbabwe, kuapishwa Ijumaa kumrithi Mugabe
Nov 22, 2017 13:02Makamu wa Rais wa Zimbabwe aliyepigwa kalamu nyekundu hivi karibuni na Rais Robert Mugabe aliyetangaza kujiuzulu hapo jana amerejea nchini akitokea Afrika Kusini.
-
Baada ya Mugabe kujiuzulu, Umoja wa Mataifa wawataka Wazimbabwe kudumisha utulivu
Nov 22, 2017 04:31Umoja wa Mataifa umewataka wananchi wa Zimbabwe kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki baada ya Rais Robert Mugabe kutangaza kujiuzulu hapo jana.
-
Wanachuo Zimbabwe waandamana dhidi ya Mugabe
Nov 20, 2017 11:06Wanachuo nchini Zimbabwe wamefanya maandamano katika kuonyesha upinzani wao kwa rais wa nchi hiyo.
-
Mugabe akataa tena kujiuzulu
Nov 19, 2017 23:58Licha ya hapo awali kutangazwa kuwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekubali kujiuzulu na kwamba angeliitumia hotuba yake kwa taifa kutangaza rasmi kuachia madaraka, lakini rais huyo kizee hakusema chochote kuhusiana na kujiuluzu kwake wakati alipolihutubia taifa jana usiku.
-
Duru za ZANU-PF: Chama tawala Zimbabwe kinapanga kumtimua Mugabe
Nov 19, 2017 04:40Viongozi wa chama tawala nchini Zimbabwe cha ZANU-PF wanatazamiwa kupitisha uamuzi wa kumuondoa uongozini Rais wa nchi hiyo na kiongozi wa chama hicho Robert Gabriel Mugabe, ambaye amekuwa akiiongoza nchi hiyo tangu ilipopata uhuru wake miaka 37 iliyopita. Hayo ni kwa mujibu wa duru mbili kutoka ndani ya chama hicho.