Mauaji na uharibifu; matokeo ya Libya kuamini na kulegeza msimamo mbele ya nchi za Magharibi/ tweet za watumiaji wa X
(last modified 2024-07-17T12:18:11+00:00 )
Jul 17, 2024 12:18 UTC
  • Mauaji na uharibifu; matokeo ya Libya kuamini na kulegeza msimamo mbele ya nchi za Magharibi/ tweet za watumiaji wa X

Libya imekumbwa na ghasia na machafuko ya kisiasa tangu mapinduzi ya mwaka 2011 ya watu wa nchi hiyo, ambayo yalipelekea kupinduliwa serikali ya Muammar Gaddafi, kwa uingiliaji kati wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya.

Kuhusu makala hii ya Parstoday, soma tweet (jumbe) hizi 9 zilizochaguliwa kutoka jumbe nyingine nyingi za watumiaji wa mitandao.

Je, ni kwa nini watu wa Libya wanazichukia nchi za Magharibi?

Kevin Scott, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anaandika kuhusiana na sababu hizo kama ifuatavyo:

Licha ya kupita zaidi ya muongo mmoja tangu nchi za Magharibi ziingilie na kuiangusha serikali ya libya, lakini bado nchi hiyo inaendelea kukabiliwa na tatizo la kutokuwa na uthabiti wa kisiasa na migawanyiko. Hivyo si jambo la kushangaza kuona kwamba nchi za Magharibi na vibaraka wake wanaendelea kutiliwa shaka na kuchukiwa katika eneo hilo.

Tweet ya Kevin Scott inazungumzia sababu za chuki ya watu wa Libya dhidi ya nchi za Magharibi

 

Sinario ya Magharibi nchini Libya

Kudzai Mutisi, mchambuzi wa kisiasa na mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, anataja katika ukurasa wake wa X sinario ya nchi za Magharibi katika kutumia vibaraka wake nchini Libya:

Vibaraka wa Magharibi nchini Libya waliitaka NATO iingilie kati na kumpindua Gaddafi. Sinario hii imerudiwa mara nyingi kote barani Afrika: Wao huwatumia vibaraka wa Magharibi katika kuhalalisha vikwazo au kulipua nchi za Kiafrika. Sasa kwa vile Gaddafi ameondoka, wanasema hilo lilikuwa kosa kubwa.

Tweet ya Kudzai Mutisi kuhusu sinario ya nchi za Magharibi nchini Libya

 

Kuongezeka masoko ya uuzaji watumwa nchini Libya baada ya uvamizi wa Magharibi

Mtumiaji wa mtandao wa X kwa jina Sudan HODL ametukumbusha kupitia tweet ya ukosoaji kuhusu kuenea kwa masoko ya watumwa huko Libya baada ya nchi za Magharibi kuivamia nchi hiyo. Anasema kwa kinaya:

Libya hivi sasa ina demokrasia kadiri kwamba hata masoko ya watumwa yameenea wazi kila sehemu. Uingiliaji wa Magharibi barani Afrika daima hutuletea uhuru na maisha mazuri zaidi.

Tweeter ta mtumiaji mtandao kuhusu kuenea masoko ya watumwa Libya baada ya uvamizi wa nchi za Magharibi.

 

Kuua maelfu ya raia wa Libya

Andrew Brophy, mtumiaji wa mtandao wa X amesema kupitia tweet kwamba uingiliaji wa Magharibi huko Libya ndiyo sababu ya kuuawa maelfu ya raia wa kawaida wa nchi hiyo. Anaandika:

Ikiwa tunatafuta mwingiliano hatari kieneo uliosababishwa na mwanadamu, itazame Libya hivi sasa. Uingiliaji wa kiwendawazimu wa nchi za Magharibi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huko umesababisha maafa ya moja kwa moja ya maelfu ya raia wasio na hatia nchini humo. Jambo hilo linatia aibu na kushtua.

Tweet ya Andrew Brophy kuhusu kuuawa maelfu ya raia wa Libya

 

Libya haijaendelea kufuatia uingiliaji wa Magharibi

Mwanaharakati wa mtandao wa kijamii wa X kwa jina Ivan_8848 anadokeza kwenye tweet yake kuhusu kutoendelea Libya na nchi nyingine ambazo zimevamiwa na Magharibi. Anasema:

Hebu itazame Libya, hakuna hata nchi moja iliyovamiwa na nchi za Magharibi, iliyopata maendeleo baada ya uvamizi.

Tweet ya Ivan kuhusu sababu za Libya kubakia nyuma kimaendeleo

 

Karim Wafa-al Hussaini, mwanahistoria, mwandishi na mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, anasisitiza katika ujumbe wa tweeter haja ya kuwa macho dhidi ya simulizi za vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu matukio ya Libya kwa kuandika:

Nashangaa kuona namna tukio hili lilivyotokea. Je, huenda ni kutokana na uingiliaji wa kijeshi wa Magharibi? Je, Libya si ni mfano mwingine wa matokeo ya maafa yanayotokana na uingiliaji wa NATO? Mbeberu ni nani? Tusipuuze nafasi ya habari ambazo zimechangia katika kubuni simulizi zilizosababisha jambo hili.

Tweet ya Karim Wafa al-Husseini kuhusu ulazima wa kuwa macho dhidi ya simulizi za uwongo za vyombo vya habari vya Magharibi.

 

Maafa na uharibifu; matokeo ya uingiliaji wa madola ya Magharibi nchini Libya

Hussein Muslim, mwanaharakati wa kisiasa na mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, anasema uingiliaji wa madola ya Magharibi nchini Libya katika miaka 12 iliyopita ndiyo sababu kuu ya maafa na uharibifu katika nchi hiyo.

Anaandika:

Mwaka 2011, Marekani na Umoja wa Ulaya ziliiteketeza Libya. Leo, maafa waliyoyasababisha ni fursa ya kuweka mipango mipya. Sasa wanajiandaa kutoa jibu la kibinadamu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba uingiliaji wa madola ya Magharibi nchini Libya katika kipindi cha miaka 12 iliyopita umesababisha maafa na uharibifu mkubwa.

Tweet ya Hussein Muslim kuhusu matokeo ya uingiliaji wa Magharibi nchini Libya

 

Uongo wa nchi za Magharibi kuhusu Bara la Afrika

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anayeitwa T'challa.eth alikuwa amechambua katika tweet yake uongo wa nchi za Magharibi kuhusu nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Libya.

Ameandika:

Ninawaza tu kwa sauti kubwa. Nchi za Magharibi zinadai kuwa zinapeleka misaada barani Afrika kwa ajili ya kutusaidia tustawi na kujiendeleza. Mtu anapaswa pia kuzungumzia kiwango cha wizi wao, lakini Wamagharibi wanatumia misaada kama kifuniko. Tazama Sudan Kusini, Kongo DR na Libya, yote ni mazao ya uingiliaji wa Magharibi katika siasa za Afrika.

Tweet ya mtumiaji kuhusu uongo wa Magharibi nchini Libya

 

Marekani imeharibu amani na utulivu wa dunia kuliko nchi nyingine yoyote ulimwenguni.

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X aitwaye Engr. Prince ameitambulisha Marekani kama nchi ambayo imeharibu zaidi amani na utulivu wa dunia kuliko nchi nyingine yoyote ulimwenguni.

Ameandika:

Marekani na washirika wake wanapaswa kujiweka mbali na masuala ya Afrika. Afrika imekomaa vya kutosha kwa ajili ya kutatua migogoro yake bila kuingiliwa na nchi za Magharibi. Tumeona Marekani ilivyofanya Libya, Syria, Iraq, Sudan na sasa Ukraine. Marekani imeharibu amani na utulivu wa dunia kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Tweet ya mtumiaji kuhusu mapigo na uvurugaji wa Marekani dhidi ya amani ya dunia

 

Tags