Kuwait yakaribisha hatua ya Denmark dhidi ya wanayoivunjia heshima Qur'ani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101524-kuwait_yakaribisha_hatua_ya_denmark_dhidi_ya_wanayoivunjia_heshima_qur'ani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait amekaribisha uamuzi uliochukuliwa na Denmark kuhusu vitendo vya kuivunjia heshima Qur'ani tukufu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 27, 2023 02:50 UTC
  • Kuwait yakaribisha hatua ya Denmark dhidi ya wanayoivunjia heshima Qur'ani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait amekaribisha uamuzi uliochukuliwa na Denmark kuhusu vitendo vya kuivunjia heshima Qur'ani tukufu.

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Sheria wa Denmark  Peter Hummelgaard alitangaza kuwa nchi yake imechukua uamuzi wa kupiga marufuku kitendo cha kuchoma moto nakala za Qur'ani tukufu, baada ya Kitabu hicho cha mbinguni kuvunjiwa heshima mara kadhaa nchini humo.

Kwa mujibu wa Al-Khaleej Online, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait Salem Abdullah Al-Jaber Al-Sabah ambapo mbali na kupongeza uamuzi wa Denmark wa kuwasilisha rasimu ya sheria inayopiga marufuku uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu, amezitolea mwito nchi zingine zinazoshuhudia kitendo hicho, zichukue uamuzi kama uliochukuliwa na serikali ya Copenhagen.

Lars Rasmussen

Al-Sabah amesisitiza kuwa, waziri wa mambo ya nje wa Denmark Lars Rasmussen amemueleza kwamba, serikali ya nchi yake imewasilisha bungeni rasimu ya sheria inayopiga marufuku kuvunjia heshima dini na itikadi mbalimbali.

Tarehe 28 Juni, Salwan Momika, mkimbizi wa Kiiraq aliuchoma moto Msahafu mbele ya msikiti wa Stockholm huku akipewa ulinzi kamili na polisi wa Sweden tarehe 28 Juni. Na mara nyingine tena aliukanyaga kanyaga Msahafu na bendera ya Iraq mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm na kupiga nara za matusi dhidi ya  Uislamu.

Mnamo 21 Julai wanachama wa kundi moja lenye chuki na Uislamu na itikadi kali nchini Denmark liitwalo Danske Patrioter waliuchoma Msahafu mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen.../