Kuwait yaungana na mataifa mengine kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani huko Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i102954-kuwait_yaungana_na_mataifa_mengine_kulaani_kuvunjiwa_heshima_qur'ani_huko_sweden
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kuwait imelaani vikali kuvunjiwa heshima tena kitabu kitakatifu cha Qur'ani huko nchini Sweden.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 02, 2023 07:12 UTC
  • Kuwait yaungana na mataifa mengine kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani huko Sweden

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kuwait imelaani vikali kuvunjiwa heshima tena kitabu kitakatifu cha Qur'ani huko nchini Sweden.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kuwait imeeleza kuwa: Kuwait imechukizwa mno na kitendo cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kwamba, kitendo hicho ambacho kimefanyika kwa ufahamuu kamili wa viongozi wa eneo husika nchini Sweden katu si cha kuhalalishika na kinapingana waziwazi na thamani na misingi yote ya utu na ubinadamu.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kuwait imetaka kuchukuliwa hatua za maana na za kivitendo ili kuzuia vitendo kama hivyo ambavyo vinahatarisha misingi ya kuishi kwa amani na vinachochea moto wa utumiaji mabavu.

 

Salwan Momika juzi alirudia tena kitendo kiovu na cha kishenzi cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu mjini Malmö kwa kibali rasmi cha Polisi ya nchi hiyo.

Katika miezi ya karibuni, Momika amechoma moto Msahafu mara kadhaa na kuibua hisia kali duniani za kukemewa, kupingwa na kulaaniwa kitendo chake hicho. Aliwahi kufanya kitendo hicho kiovu kwa kibali rasmi cha Polisi ya Sweden tena mbele msikiti mkuu wa Stockholm hata katika moja ya Sikukuu kubwa ya Waislamu ya Idul-Adhha iliyosadifiana na tarehe 28 Juni mwaka huu.

Serikali na viongozi wa Sweden ambao wamedai mara kadhaa kuwa watachunguza vitendo hivyo kisheria na kisiasa wanaendelea kuunga mkono jinai hizo dhidi ya Uislamu na kuzidi kuchochea hisia za Waislamu duniani.