Askari Mzayuni awabembeleza wanamapambano wa Palestina wasimuue + VIDEO
Wanamapambano wa Palestina wamesambaza mkanda wa video unaomuonesha askari wa Tel Aviv akitetemeka mwili mzima huku akiwaomba kwa kubembeleza wanamapambano wa Palestina wasimuue.
Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, wanamapambano wa Palestina jana (Alkhamisi) jioni walisambaza mkanda wa video unamuonesha askari huyo wa Israel waliyemteka nyara akiwabembeleza wanamapambano hao ili wasimfanye chochote. Askari huyo anaonekana akitetemeka mwili mzima wakati anaomba asichukuliwe hatua na wanamapambano hao.
Mkanda huo wa video unamuonesha askari huyo akiomba msamaha kutokana na jinai alizofanya yeye na askari wenzake wa Israel dhidi ya Wapalestina. Anasikika akisema: "Nakuombeni msiniue. Nakiri sisi (Wazayuni) ni taifa la watenda jinai."
Tangu ilipoanza operesheni ya kishujaa na ya kihistoria ya #Kimbunga_cha_al-Aqsa siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Agosti, 2023, utawala wa Kizayuni wenyewe umekiri kuwa zaidi ya Wazayuni 1,300 wameshaangamizwa na mamia ya wengine wamejeruhiwa. Idadi ya Wazayuni waliotekwa nyara na wanamapambano wa Palestina haijulikani. Wanamuqawama wa Palestina wanasema idadi ya mateka walio nao ni kubwa mno ya unavyoweza kutasawari utawala wa Kizayuni wa Israel.
Gilad Erdan, mwakilishi wa kudumu wa utawala wa Kizayuni katika Umoja wa Mataifa amedai kuwa, viongozi wa Israel wanaamini kwamba wanamuqawama wa Palestina wanawashikilia mateka Wazayuni 150.
Amedai kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni wana matumaini watawakomboa mateka hao lakini kuweko mateka hao huko Ghaza hakutowazuia kufanya mashambulizi kwenye maeneo mbalimbali ya ukanda huo.
Afisa huyo wa ngazi za juu wa utawala wa Kizayuni amedai pia kuwa, wanavyoamini wao ni kwamba kuna baina ya mateka 100 hadi 150 wa Kizayuni ndani ya mikono ya Wapalestina na wakati huo huo amekiri kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa Wazayuni kutekwa nyara kwa idadi kubwa kama hiyo.
Lakini kama walivyonukuliwa wanamapambano wa Palestina, idadi ya mateka hao ni kubwa zaidi ya wanavyodhania viongozi wa Israel.