HAMAS: Borrell anapindua ukweli wa mambo kuhusu Ghaza
(last modified Mon, 13 Nov 2023 13:44:29 GMT )
Nov 13, 2023 13:44 UTC
  • HAMAS: Borrell anapindua ukweli wa mambo kuhusu Ghaza

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, matamshi ya mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya dhidi ya makundi ya muqawama ni kupindua uhakika wa mambo na ni kujaribu kufunika jinai za utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema hayo leo Jumatatu na kuongeza kuwa, matamshi ya Josep Borrell, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya kuhusu makundi ya muqawama wa Kiislamu, ni upotoshaji wa wazi wa uhalisia wa mambo. 

Katika matamshi yake ya hivi karibuni, Borrell ameilaumu harakati ya HAMAS na kuunga mkono waziwazi jinai za utawala wa Kizayuni kwa madai kuwa eti Israel ina haki ya kujilinda.

 

Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya HAMAS imejibu haraka upotoshaji huo wa Umoja wa Ulaya kwa kusema kuwa, tuhuma zinazotolewa na Josep Borrell kwamba makundi ya muqawama yanatumia hospitali kama kambi za kijeshi hayana ukweli wowote bali ni katika juhudi zilizofeli za kujaribu kukingia kifua jinai za kuchupa mipaka zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watoto, wanawake, vizee na wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hizo za Ghaza.

Taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeongeza kuwa, tuhuma hizo za mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya dhidi ya HAMAS ni uungaji mkono wa wazi wa jinai za Israel dhidi ya binadamu na ni upotoshaji wa uhalisia wa mambo.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya HAMAS imesema: Tunapinga vikali matamshi ya hatari ya Borrell ambayo yamepuuza picha zote, ushahidi wote na ripoti zote za kimataifa kuhusu jinai zinazofanywa na Wazayuni huko Ghaza. Tunamtaka Borrell afute haraka matamshi yake yasiyokubalika kabisa. 

Tags