Kudhoofika nafasi ya Marekani miongoni mwa nchi za Kiarabu
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni katika nchi kadhaa za Kiarabu kuhusu Marekani umeonyesha kuwa fikra za waliowengi katika nchi za Kiarabu zimekuwa hasi sana kutokana na uungaji mkono wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni katika vita dhidi ya Gaza.
Taasisi kwa jina la Washington Institute for Near East Policy imetangaza kuwa matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na kundi huru la utafiti kwa jiana la Jordanian Civil Society Studies yameonyesha namna Washington inavyoukingia kifua utawala wa Israel katika mashambulizi yake dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza. Mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza yamedhoofisha pakubwa ushawishi wa Marekani miongoni mwa nchi za Kiarabu kuwahi kushuhudiwa katika historia.
Uchunguzi huu wa maoni uliofanywa huko Iraq, Syria, Jordan, Misri, Lebanon na Palestina wakati huo huo umeonyesha kuongezeka uungaji mkono kwa wapinzani wa stratejia ya Marekani yaani China, Russia na Iran.
Kwa wastani yaani asilimia 40 ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo wa maopni wanaamini kuwa Iran imekuwa na athari chanya katika vita vya Gaza. Huko Misri asilimia 50 na nchini Syria asilimia 52 ya watu waliotoa maoni yao katika uchunguzi huo wa maoni wanaamini kuwa Iran imekuwa na nafasi chanya katika vita vya Gaza.