Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa wafikia 501
(last modified 2024-01-04T03:10:17+00:00 )
Jan 04, 2024 03:10 UTC
  • Idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa wafikia 501

Utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza kuwa, idadi ya askarii wake waliouawa hadi sasa tangu ilipototekkelezwa operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa imefikia 501.

Kwa mujibu wa duru za Kiizayunii idadii hiyo imeongezeka baada ya askari mwingiine wa Israel kuuawa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, idadi ya askari wa utawala wa Kizayuni waliaongamizwa tangu jeshi la Israel lilipoanzisha operesheni ya nchi kavu dhidi ya uukanda wa Gaza imefikia 175.

Utawala dhalimu wa Israel ambao umeshindwa kwenye medani za mapambano, umeamua kumalizia hamaki zake kwa kuua watoto wadogo, wanawake, vizee na raia wa kawaida huko Gaza.

Katika upande mwingine, imeelezwa kuwa, wakati mfumo wa afya ya akili wa Israel unakabiliwa na hatari ya kuporomoka, madaktari wa magonjwa ya akili wanaondoka kuelekea Uingereza kutafuta hali bora zaidi ya maisha.

 

Kugura huko kwa madaktarii wa afya ya akili kunakuja wakati mahitaji ya huduma za afya ya akili huko Israel yanaongezeka kutokana na vita vya Gaza, na kwamba wiki iliyopita wakuu wa vituo vya afya ya akili walituma barua kwa Mdhibiti wa Serikali, Matanyahu Englman, wakionya kwamba "mfumo wa afya ya akili wa Israel unakaribia kusambaratika kabisa.”

Tarehe 7 Oktoba 2023, makundi ya muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza kusini mwa Palestina dhidi ya maeneo ya utawala unaoikalia kwa mabavu  Quds, na  ili kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake na kukomesha operesheni za makundi ya Kipalestina, utawala huo umekuwa ukishambulia kinyama maeneo ya makazi, matibabu na kitamaduni ya Ukanda wa Gaza.

Tags