Wanajeshi 560 wa Israel wameshaangamizwa hadi hivi sasa Ghaza
Jeshi la utawala wa Kizayuni ambalo ni maarufu kwa kuchuja mno habari limesema katika taarifa yake ya jana kwamba, hadi hivi sasa wanajeshi 560 wa Israel wameshaangamizwa tangu vilipoanza vita vya Ghaza, tarehe 7 Oktoba, 2023.
Shirika la habari la FARS limetangaza habari hiyo na kusema kuwa, takwimu zinazotolewa na jeshi la Israel ni ndogo mno ikilinganishwa na idadi hasa ya maafa na hasara linazopata jeshi hilo huko Ghaza.
Tangu vilipoanza vita vya Ghaza, baada ya operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa iliyoendeshwa kishujaa na wanaharakati wa Palestina, kila siku jeshi la utawala wa Kizayuni linatangaza kwa idadi ndogo mno wanajeshi wake walioangamizwa. Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa ya tarehe 7 Oktoba 2023 iliyoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa pigo kubwa la kisiasa, kiuchumi, kiujasusi na kiusalama kwa Israel.
Wazayuni wanachuja mno habari zao kutokana na idadi kubwa ya maafa wanayopata wanajeshi wa Israel huko Ghaza na kiwewe chao cha kuhofia kuripuka hasira za walowezi wa utawala wa Kizayuni.

Katika kuendelea kuchuja mno habari zake, utawala wa Kizayuni umedai kuwa, kwenye kipindi cha saa 24 zilizopita, wanajeshi wake wengine watatu wameangamizwa huko Ghaza.
Vilevile usiku wa kuamkia leo Alkhamisi, jeshi la utawala wa Kizayuni limethibitisha habari ya kuangamizwa Meja Jenerali Yitzhar Hofman, aliyekuwa kaimu wa kamanda mkuu wa kikosi maalumu cha mauaji cha utawala wa Kizayuni kiitwacho Shaldag.
Kuangamizwa afisa huyo wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni kumezidi kuonesha kuwa, hasara wanazopata wanajeshi vamizi na makatili wa Israel huko Ghaza ni kubwa mno. Makamanda wa Israel wanaendelea kuangamizwa katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni ulikuwa unadai kwamba umedhibiti kila kitu hasa maeneo ya kaskazini mwa Ukanda huo.