HAMAS: Tumeangamiza askari 12 wa Israel katika 'operesheni tata' Jabalia, Ghaza
Izzuddin-al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa wapiganaji wake wamewaangamiza wanajeshi 12 wa Israel katika eneo lililozingirwa la kaskazini mwa Ghaza.

Wakati huohuo, Brigedi za Abu Ali Mustafa, kundi jingine la Muqawama la Palestina, limetangaza kuwa limefanya shambulio la roketi lililolenga vikosi vya jeshi la Kizayuni mashariki mwa kambi ya Jabalia.
Kundi la brigedi ya Nasser Salahuddin nalo pia limetangaza kuwa katika operesheni ya pamoja na vikosi vya al-Qassam, wameripua gari la kijeshi la askari wa jeshi la Kizayuni kwa bomu nata na kwamba askari waliokuwemo ndani yake wameuawa au kujeruhiwa.
Katika taarifa nyingine, kundi hilo limetangaza kuwa katika operesheni ya pamoja na Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina, limeshambulia eneo la walowezi wa Kizayuni wa Sdirut karibu na Ukanda wa Ghaza kwa makombora 2 aina ya 107.../