Askari 7 wa Israel waangamizwa, 49 wajeruhiwa katika mapigano na wanamuqawama wa Hizbullah
(last modified Thu, 17 Oct 2024 03:26:28 GMT )
Oct 17, 2024 03:26 UTC
  • Askari 7 wa Israel waangamizwa, 49 wajeruhiwa katika mapigano na wanamuqawama wa Hizbullah

Askari wasiopungua saba wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameripotiwa kuangamizwa katika mapigano na harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwenye mpaka wa kusini wa nchi hiyo na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Vyombo vya habari vya Israel vimesema, askari hao waliuawa jana Jumatano katika mapigano yaliyotokea karibu na vijiji vya mpakani mwa Lebanon vya Aita al-Shaab.
 
Ripoti za vyombo hivyo zimebainisha kuwa, wanajeshi wengine wengi walijeruhiwa, 17 kati yao wakiwa mahututi, wakati wa makabiliano hayo yaliyofuatia mashambulizi ya kuvizia ya Hizbullah, na kuongeza kwamba kuna udhibiti mkali uliowekwa na jeshi la Israel karibu na eneo yalipojiri mapigano hayo.
 
Hapo awali, ripoti zilionyesha kuwa wanajeshi wapatao 49 waliojeruhiwa wamehamishwa na kupelekwa hospitali.
Wanamuqawama wa Hizbullah

Imeelezwa kuwa majeruhi 44 walisafirishwa kwa ndege hadi hospitali katika mji wa Haifa katika sehemu ya kaskazini ya eneo hilo.

 
Hospitali ya Rambam katika mji huo imeripoti kuwepo kwa majeruhi wengi na kutoa wito wa kupatiwa wafanyakazi wa ziada wa sekta ya tiba baada ya helikopta nane kutua hapo zikiwa na majeruhi.
 
Kwa mujibu wa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah, makabiliano hayo yalishuhudia wapiganaji wa harakati hiyo wakiingia kwenye mapigano makali ya ana kwa ana na wanajeshi wa Israel kwa kutumia aina mbalimbali za bunduki.
 
Mapigano hayo yameripotiwa kuendelea huku kukiwa na mashambulizi makubwa ya risasi na harakati za helikopta katika eneo hilo.
 
Operesheni hiyo ya kuvizia iliyotekelezwa na Hizbullah imevilenga vikosi vya jeshi la Kizayuni vya Brigedi ya Golan.../
 
 

Tags