Amnesty International yaitaka mahakama ya ICC kuchunguza jinai za Israel Rafah
(last modified Mon, 27 May 2024 11:57:54 GMT )
May 27, 2024 11:57 UTC
  • Amnesty International yaitaka mahakama ya ICC kuchunguza jinai za Israel Rafah

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuchunguza jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah katika Ukanda wa Gaza.

 Erika Guevara Rosas, Mkurugenzi Mkuu wa Amnesty International amesema: Jinai za utawala wa Israel zinaonyesha mwelekeo wa wazi wa mashambulizi ya jeshi la utawala huo katika kipindi cha miezi saba na nusu, ambayo yalikiuka sheria za kimataifa na kuwaua raia wote wa Palestina. Uchunguzi huo unaonyesha kuweko jinai zinazofanywa na Israel huko Rafa, imeongeza taarifa hiyo ya Amnesty International.

Aidha amesema, shirika hilo lilifanya uchunguzi huru kuhusu mashambulizi haya matatu na kuwahoji manusura 17 na mashahidi na kutembelea hospitali ambapo majeruhi walitibiwa.

 

Hayo yanaripotiwa huku, Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ ikiwa tayari imeuamuru utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe mara moja mashambulizi yake katika mji wa kusini mwa Ghaza wa Rafah na kujiondoa katika eneo hilo, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini ikiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari, na kuielezea hali hiyo kuwa ni hatari kubwa kwa wakazi wa Palestina.

Katika upande mwingine, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilitangaza Jumatatu iliyopita kwamba imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa Vita Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala wa kibaguzi wa Israel kwa tuhuma za uhalifu wa kivita wanaoutenda huko ukanda wa Gaza.

Tags