Hamas: Utawala wa Kizayuni haujui lolote isipokuwa kuuwa wanawake na watoto
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiisamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari haujui lolote jingine isipokuwa kuwashambulia na kuwauwa wanawake na watoto wasio na hatia.
Izzat al Risheq ameashiria kuendelea mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza na kusema: Juzi ijumaa utawala wa Kizayuni uliwauwa shahidi watu 16 wa familia moja katika kitongoji cha Az-Zawayda katikati mwa Ukanda wa Gaza ikiwa ni katika kuendelea mashambulizi ya Israel dhidi ya makazi ya wakimbizi wa Kipalestina.
Al Risheq ameongeza kuwa: Katika hali ambayo muqawama wa Palestina unamshambulia adui Mzayuni na silaha zake; jeshi la Kizayuni linaendelea kuwashambulia wanawake na watoto na kuharibu mahitaji yote ya lazima ya maisha ya mwanadamu katika Ukanda wa Gaza.
Afisa huyo wa Hamas amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa jinai za utawala wa Kizayuni na kusema jamii ya kimataifa inatazama tu jinai hizo bila kuchukua hatua zozote madhubuti ili kusimamishwa vita huko Ukanda wa Gaza. Uchunguzi wa maoni uliofanywa na televisheni ya 12 ya utawala wa Kizayuni umeonyesha kuwa asilimia 63 ya walowezi wa Kizayuni wanataka kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita Ukanda wa Gaza kati ya viongozi wa Tel Aviv na muqawama wa Palestina.
Mazungumzo ya Alhamisi iliyopita huko Doha kati ya Hamas na utawala wa Kizayuni kwa upatanishi wa Misri na Qatar na kuhudhuriwa na Marekani kwa ajili ya kufikia mapatano ya kusimamisha vitaUkanda wa Gaza na kubadilishana mateka baina ya pande mbili hayakuzaa matunda.