Duru mpya ya mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Lebanon
Jeshi la utawala katili wa Israel limeendeleza jinai zake kwa shambulia kwa mabomu maeneo ya raia mashariki mwa Lebanon.
Kwa mujibu shirika la habari la IRNA, ndege za kivita za utawala huo katili asubuhi ya leo zimeshambulia maeneo ya Baalbek, Dorres, Al-Jamaliyah, Brital, Al-Khidr, Amhz na Shaath na Nahle, na huko mashariki mwa Lebanon.
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni pia zimelenga jengo lenye ghorofa sita katika eneo hilo la Al-Ghobeiri lililoko katika viunga vya kusini mwa Beirut huko Lebanon.
Televisheni yya Al-Mayadeen ya Lebanon imeripoti kuwa ghorofa 3 za jengo hilo zimeharibiwa vibaya mno.
Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza katika taarifa yake kwamba, Walebanon 558, wakiwemo watoto 50 na wanawake 94 wameuawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kinyama ya ndege za kivita za jeshi la Israel katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.