UN yakosoa tena jinai za utawala ghasibu wa Israel
Umoja wa Mataifa umesisitiza tena misimamo yake kuhusu jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina siku moja baad aya utawala huo kupinga matamshi ya Katibu Mkuu wa umoja huo ddhidi ya mienendo ya Israel.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesisitiza kuwa baada ya miaka mingi ya subira na matumaini ya kutimiziwa ahadi walizopewa, wananchi wa Palestina sasa wamepoteza matumaini na kuchoshwa na siasa na sera za ukandamizaji wa utawala ghasibu.
Ban Ki-moon ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kutetea Haki za Wapalestina ameashiria miaka zaidi ya 50 ya uvamizi wa Israel na kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na kusema, Wapalestina hususan vijana wamepoteza matumaini baada ya kusubiri kutimiziwa ahadi za mkataba wa Oslo kwa miongo kadhaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia amesisitiza tena misimamo thabiti ya umoja huo ya kupinga vikali ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Amesema ujenzi wa vitongozi hivyo unakiuka sheria za kimataifa na ni tishio kwa juhudi za utatuzi wa kadhia ya Palestina.