Msemaji wa Hizbullah auawa shahidi katika shambulio la kinyama la Israel
(last modified Sun, 17 Nov 2024 14:49:06 GMT )
Nov 17, 2024 14:49 UTC
  • Msemaji wa Hizbullah auawa shahidi katika shambulio la kinyama la Israel

Mohammad Afif, afisa wa habari wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameuawa shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni huko Ras al-Naba, Beirut mji mkuu wa Lebanon.

Kanali ya Televisheni ya al-Jazeera iimeinukuu duru moja ya kiusalama na kutangaza kuwa, msemaji huuyo wa Hizbullah ameuawa leo katika mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya eneo la Ras al-Naba Beirut.

Wakati huo huo, Ali Hijazi, Katibu Mkuu wa Chama cha Arab Socialist Ba'ath, ameiambia Kanali ya Televisheni ya Al-Mayadeen kwanmba, shambulio dhidi ya ofisi yetu lilienda sambamba na vitisho vya mfululizo dhidi yetu tangu mwanzo wa vita. Jengo lililolengwa lilitumiwa na chama. Hakukuwa na raia katika jengo hili. Tulifanya mikutano mingi katika jengo hili wakati wa vita na ilijulikana kwa kila mtu. Mmoja wa watu waliokamatwa miezi miwili iliyopita alikiri kwamba alikuwa wakala wa kupiga picha kutoka makao makuu ya Chama cha Baath.

Huku akithibitisha kuuawa shahidi kwa afisa wa habari wa Hizbullah Mohammad Afif, Katibu Mkuu wa Chama cha Arab Socialist Ba'ath amese: Mohammad Afif alikuwa kwa bahati mbaya kwenye jengo lililolengwa na aliuawa shahidi. Lengo la mashambulizi haya ni kunyamazisha vyombo vya habari na sauti ya kisiasa ya muqawama kwa sababu inawaudhi sana. Tunaunga mkono muqawama na bila shakka muqawama huu utashinda uwe siisi tupo au hatupo.

Harakati ya Hizbullah badoo haijathibitisha rasmi kuuawa shahidi afisa wakke huyo wa vyombo vya habari.