Amnesty yatiwa wasiwasi na ukandamizaji na kamatakamata Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11953-amnesty_yatiwa_wasiwasi_na_ukandamizaji_na_kamatakamata_uturuki
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza masikitiko yake juu ya kukithiri ukandamizaji, kamata kamata na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Uturuki, baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililofeli.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 25, 2016 08:06 UTC
  • Amnesty yatiwa wasiwasi na ukandamizaji na kamatakamata Uturuki

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza masikitiko yake juu ya kukithiri ukandamizaji, kamata kamata na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Uturuki, baada ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililofeli.

Lama Fakih, Mshauri Mkuu wa masuala ya mizozo katika shirika la Amnesty International ameiambia shirika la habari la Russia Today kuwa, licha ya kutokuwepo ushahidi, lakini vyombo vya dola vinawakandamizi watu wanaodhaniwa kuwa walihusika na mapinduzi hayo yaliyofeli. Amesema baadhi ya mateso wanayoyapitia watuhumiwa hao au mtu yeyote anayeonekana kuwaunga mkono ni kutandikwa, kunyimwa huduma za matibabu, kunyimwa chakula na maji huku baadhi yao wakinajisiwa.

Nembo ya Shirika la Msamaha Duniani

 

Mshauri Mkuu wa masuala ya mizozo wa Amnesty International ameongeza kuwa, katika hali ya ambayo serikali ya Ankara ina jukumu la kudhamini usalama wa taifa, lakini wajibu huo haufai kukiuka haki za msingi za watuhumiwa au kutumika kama kisababu cha kuwalenga wakosoaji na wapinzani wa serikali.

Haya yanajiri siku chache baada ya serikali ya Morocco kuonyesha wasiwasi wake kuhusiana na kamatakamata inayoendelea nchini Uturuki baada ya kujiri mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli.

Rais wa Uturuki Recep Teyyip Erdogan

 

Katika jaribio la mapinduzi ya kijeshi dhidi ra serikali ya Rais Recep Tayyip Erdoğan, ambalo lilitekelezwa na baadhi ya askari wa jeshi la Uturuki, karibu watu 300 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Kwa mujibu wa duru za habari nchini Uturuki karibu watu 50 elfu kati ya maafisa wa serikali, wametiwa mbaroni na kusimamishwa kazi kufuatia tukio hilo.