Mamluki wa Jolani wapigana na vikosi vya Wakurdi, Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121674-mamluki_wa_jolani_wapigana_na_vikosi_vya_wakurdi_syria
Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kujiri mapigano kati ya mamluki wa utawala wa Jolani na wanamgambo wa Kikurdi, QSD, katika viunga vya Deir ez-Zor.
(last modified 2025-01-20T11:07:17+00:00 )
Jan 20, 2025 11:07 UTC
  • Mamluki wa Jolani wapigana na vikosi vya Wakurdi, Syria

Vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kujiri mapigano kati ya mamluki wa utawala wa Jolani na wanamgambo wa Kikurdi, QSD, katika viunga vya Deir ez-Zor.

Televisheni ya Syria imetangaza leo kuwa, mapigano ya silaha yamejiri kati ya mamluki wenye mfungamano na utawala wa Jolani, kamanda wa kundi la Hay'at Tahrir al-Sham na Vikosi vya Kidemokrasia vya Wakurdi wa Syria (QSD) katika eneo la kati ya Abu Hamam na Gharanij mashariki mwa mji wa Deir ez-Zor mashariki mwa Syria. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mamluki wenye mfungamano na utawala wa Jolani walisonga mbele kuelekea mikoa ya kaskazini mashariki na mashariki mwa Syria tangu jana, maeneo ya mashariki ya mji wa Halab na katika maeneo ya bwawa la Tishrin wakiwa na zana zao za kivita. 

Jana, Mazloum Abdi, kamanda wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Wakurdi wa Syria (QSD) alitangaza kuwa wapiganaji wa Kikurdi hawatasalimisha silaha zao na kusisitiza kuwa: "Tunashuhudia juhudi za Uturuki za kuzidisha ushawishi wake katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Syria kwa sababu Ankara inapanga kuyatwaa maeneo hayo na kuyaunganisha na yake yaliyo chini ya udhibiti wake kwa kulikalia kwa mabavu eneo la Ain al-Arab.