Rais wa Misri kwa mara nyingine apinga kuhamishwa Wapalestina Gaza
(last modified Sat, 26 Apr 2025 02:38:11 GMT )
Apr 26, 2025 02:38 UTC
  • Rais wa Misri kwa mara nyingine apinga kuhamishwa Wapalestina Gaza

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi jana Ijumaa alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi hiyo ya Kiarabu "inapinga kikamilifu" kufurushwa Wapalestina kwenye makazi yao na kuhamishiwa katika nchi nyingine, na kuvitaja vita vya Gaza kuwa "janga la kibinadamu."

Akihutubia taifa kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa kuadhimisha kumbukumbu ya ukombozi wa Peninsula ya Sinai, al-Sisi ametaka "kusitishwa haraka na mara moja mapigano", kuachiliwa huru mateka na wafungwa, na kufikishwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa bila vizuizi.

Amesema vita vinavyoendelea Gaza, ambavyo vimeua makumi ya maelfu ya Wapalestina kwa mujibu wa maafisa wa afya katika eneo hilo linaloongozwa na Harakati ya Muqawama ya Hamas, ni tukio ambalo "litatia doa rekodi za historia."

Sisi amesema kuwa, Misri imesalia na nia ya kuzuia "kufifilizwa kadhia ya Palestina" huku akisisitiza kuwa, amani ya kudumu inaweza kupatikana tu kwa kuanzishwa taifa huru la Palestina kwa kuzingatia "maazimio halali wa kimataifa."

Hotuba ya jana ya Sisi ilitolewa kwa mnasaba wa kuadhimisha Siku ya Ukombozi wa Sinai, kukumbuka kuondoka vikosi vya Israel katika eneo hilo mnamo 1982, kufuatia kusianiwa Mkataba wa amani wa Camp David na Israel mnamo 1979.

Takriban Wapalestina 2,000 wameuawa na wengine zaidi ya 5,200 kujeruhiwa tangu Israel ilipoanzishwa upya mashambulizi yake ya anga na ardhini mnamo Machi 18 huko Gaza, wakati jumla ya vifo vya Wapalestina tangu Oktoba 2023 vikipindukia 51,000, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Wizara ya Afya ya Gaza. Israel pia imezuia kuingia misaada ya kibinadamu Gaza tangu Machi 2