UNICEF yaonya tena dhidi ya mauaji ya Watoto Gaza
(last modified Sun, 08 Jun 2025 03:47:03 GMT )
Jun 08, 2025 03:47 UTC
  • UNICEF yaonya tena dhidi ya mauaji ya Watoto Gaza

Msemaji wa Mfuko wa Kuhuduumia Watoto wa Uumoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina ametangaza kuwa: Mauaji ya watoto wasio na hatia na yanayoendelea Gaza yamechochea hasira ya walimwengu.

Kazem Abu Khalaf ameiambia Kanali yay Televisheni ya Al Jazeera Qatar: Hakuna uhalali wa kuua watoto huko Gaza. Watoto 50,000 wameuawa au kujeruhiwa hadi sasa.

Msemaji wa UNICEF ameonya kuwa, hakutakuwa na amani katika eneo hilo kwa mauaji ya watoto na uharibifu wa Gaza kwa njia hii.

Alifafanua: Kutumia njaa kama silaha kunachukuliwa kuwa uhalifu wa kivita na tunaitaka Marekani ichukue hatua kupeleka msaada wa chakula na dawa.

Abu Khalaf aliongeza: "Tunaendelea kutoa shinikizo la kisiasa kwa ajili ya kupeleka misaada, lakini hali ya Gaza inazidi kuwa mbaya kila siku."

Mashirika na asasi mbalimbali za kimataifa zimeendelea kuonya kuhusiana na hali mbaya inayowakabili watoto katika Ukanda wa Gaza.

Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa, watoto wa Gaza sio tu wanakabiliwa na kifo kutokana na shambulio mashambulio ya mabomu, bali pia maisha yao yanakabiliwa na kifo kutokana na njaa, ukosefu wa huduma za matibabu, na kuenea kwa magonjwa kutokana na ukosefu wa maji ya kunywa, na kwa upande mwingine, misaada ya kibinadamu kwa eneo hilo haiwezekani.

Licha ya miito ya kila upande ya kutaka kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza, lakini utawala haramu wa Israel ukipata himaya na uungaji mkono wa Marekani na washirika wake umeendelea kukwamisha ufikiwaji misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.