Yemen yaanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127706-yemen_yaanzisha_mashambulizi_mapya_dhidi_ya_israel
Ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika katika maeneo mengi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya jeshi la Yemen kuvurumisha makombora kuelekea utawala wa Kizayuni ili kulipiza kisasi vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea kufanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro.
(last modified 2025-06-28T07:36:48+00:00 )
Jun 28, 2025 07:36 UTC
  • Yemen yaanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Israel

Ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika katika maeneo mengi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya jeshi la Yemen kuvurumisha makombora kuelekea utawala wa Kizayuni ili kulipiza kisasi vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea kufanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa, mashambulizi mapya ya jeshi la Yemen mapema leo yamepelekea kusikika sauti za ving'ora katika maeneo ya Beersheba, Dimona na katika vitongoji vingine vya walowezi kusini mwa ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu.

Jeshi la Israel limedai kuwa mifumo yake ya kukabiliana na makombora inafanya kazi za kutungua makombora hayo dhidi ya utawala huo. 

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen juzi Alhamisi alisema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo ya Kiarabu vimevurumisha makombora ya balistiki na ya hypersonic 309 pamoja na droni dhidi ya Israel tangu katikati ya mwezi Machi mwaka huu kama sehemu ya marhala ya pili ya oparesheni ya kijeshi ya jeshi la Yemen dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni. 

Abdul Malik al Houthi amesema kuwa makombora 25 na droni zilirushwa mwezi huu pekee katika kile alichokitaja kuwa Oparesheni bora za kijeshi za kuiunga mkono Gaza."

Amesisitiza kwa mara nyingine kwamba Bahari Nyekundu ya kimkakati bado imefungwa kwa meli zinazoelekea Israel.