Afisa wa UN: Israel inawasababishia njaa kwa makusudi watu wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128650-afisa_wa_un_israel_inawasababishia_njaa_kwa_makusudi_watu_wa_gaza
Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu anasema utawala wa Israel unawaua kwa makusudi watu wa Gaza na kupuuza maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kusitisha jinai zake.
(last modified 2025-07-23T00:20:46+00:00 )
Jul 23, 2025 00:20 UTC
  • Afisa wa UN: Israel inawasababishia njaa kwa makusudi watu wa Gaza

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu anasema utawala wa Israel unawaua kwa makusudi watu wa Gaza na kupuuza maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kusitisha jinai zake.

Jonathan Whittall ameeleza kuwa, Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wamenusurika na mashambulizi ya mabomu na risasi sasa wanataabika kwa baa la njaa. Amesema, Jumatatu wiki hii wanajeshi wa Israel, kwa mara nyingine tena, waliufyatulia risasi umati wa watu waliokuwa wakisubiri misaada ya chakula. 

Whittall ameongeza kuwa, watu milioni 2.1 katika Ukanda wa Gaza hawana chakula cha kutosha wala maji ya matumizi ili kuweza kuishi. 

Amesisitiza kuwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Israel iliamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutowasababishia kwa makusudi wananchi wa Palestina hali ambayo itapelekea kuzorota hali yao ya kimwili.   

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) huko Palestina amesema: Israel pia iliamriwa kruhusu haraka iwezekanavyo misaada ya kibinadamu kuingia kwa wingi Ukanda wa Gaza kupitia vivuko vya nchi kavu kwa kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa. 

"Vifo na mateso haya yanazuilika", ameeleza Jonathan Whittall.